Hii kauli imekuwa ikisikika sana sehem nyingi hasa sehem zile ambazo tunaenda kwa ajili ya Kupata Huduma Mbali Mbali.
Mm juzi nliingia Bar Moja Maarufu Pale Kinondoni(Uhuru Peak) kwa ajili ya Kifungua Kinywa. Nikaagiza Mtori. Baada ya kumaliza na kulipia, nkarudishiwa Chenji yangu huku nikijulishwa kuwa Samahani utanidai Tsh400. Simple as that kama vile tunafahamiana. Kumbe Maskini mm ni Mpita Njia tu.
Sasa suali linakuja. Kwa Mtindo huo!? Wakija watu 10 akawalaghai kwa Mtindo huo!? Hajaendesha Maisha yake Nje ya Mshahara!?
Hata kwenye club kubwa kubwa wakishakujua kuwa ww ni Mzungusha round, kauli kama hizo hazikosekana.
Je! Hawa wahudumu hufanya hivi tu kwa kisingizio kutokana na Mazoea na tabia ambayo wamejijngea na ishaota Mizizi!?
Namfagilia Mzee Mmoja nliwahi kukutana naye Dukani siku moja. Akapewa Maneno kama hayo, kuwa utanidai 100. Mzee aliicharuka kweli kweli. Mbona 100 alikuwa nazo nyingi dukani pale na akatoa.
Hapo ndipo nlipo amini kuwa ni katabia ambako wamejijengela hawa wadhalimu.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums