Elvis Legacy
JF-Expert Member
- Aug 10, 2017
- 4,941
- 7,955
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hatari kwelMajira ya saa saba usiku nikiwa nimetoka bar akili ikiwa imeshachoka kutokana na balimi tisa nilizopiga nilikuwa nakatiza mtaa wa mkwajuni karibu na makaburi ya wahenga wa mtaa huo uliopo maeneo ya Tabata Kajiungeni. Ghafla nilikutana na mzee mmoja wa makamo aliyeniangalia usoni kwa kunikazia macho kana kwamba ananidai kisha hakuongea chochote zaidi tu ya kuguna na kutema mate chini kisha akanipa mgongo na kuchikichia kichakani. Kwa mawazo yangu nilihisi yule mzee atakuwa mwanga tu.
Punde kidogo vijana wawili wakiwa wamevaa mashuka mmoja shuka jeusi na mwingine shuka jekundu walitokea mwelekeo ule ule aliotokea yule mzee wakiwa wanaongozana. Mmoja alikuwa amebeba mshumaa unaowaka na mwingine amebeba njiwa. Baada ya kufika karibu na mimi wa kwanza aliniuliza "Upo salama wewe?" sikumjibu chochote, nakumbuka nilikuwa natafuta tusi la kumpa lakini sikulipata kwa haraka, mdomo kila nikiufungua ulikuwa unanisaliti, nilibaki tu nayumba yumba huku nikichezesha mikono kana kwamba kuna kitu nataka kuongea lakini sikikumbuki, wakati nipo katikati ya hiyo hali basi yule kijana wa wa pili akaniuliza swali jingine""Shetani ameelekea wapi?" Sikuwa na jibu la haraka haraka kumpa maana nilifikiri amekosea kuuliza swali. Akauliza tena "Umemwona Shetani?" Safari hii nililisikia swali vizuri. Ikabidi niache kuyumba nikae kikakamavu kama vile askari kamwona mkuu wa kikosi.
Kwa sauti ya chini nikanyanyua kinywa nikawaambia "Sijamwona kwani vipi?" Ghafla bin vuu wakatimua mbio kila mmoja na mwelekeo wake aliyebeba mshumaa aliutupa chini na kuelekea alipo elekea yule mzee karibu na vichaka akapotea yule mwingine alirudi alipotokea akiwa amemshikilia yule njiwa pasipo kumwachia. Nilishikwa na butwaa nisijue nikimbilie wapi. Maana safari yangu ilikuwa imeingia mkosi. Kwa takribani sekunde tano hivi kichwa hakikufanya maamuzi yoyote ndipo niliamua kujipiga makofi mawili matakatifu pombe ipotee. Ile natafuta njia ya kukimbilia mara nikamuona yule mzee aliyenipita mara ya kwanza anatokea kichakani huku anakimbia.
Eee bwana eeh, nyuma yake kulikuwa na kundi la watu linamkimbiza.....
Majira ya saa saba usiku nikiwa nimetoka bar akili ikiwa imeshachoka kutokana na balimi tisa nilizopiga nilikuwa nakatiza mtaa wa mkwajuni karibu na makaburi ya wahenga wa mtaa huo uliopo maeneo ya Tabata Kajiungeni. Ghafla nilikutana na mzee mmoja wa makamo aliyeniangalia usoni kwa kunikazia macho kana kwamba ananidai kisha hakuongea chochote zaidi tu ya kuguna na kutema mate chini kisha akanipa mgongo na kuchikichia kichakani. Kwa mawazo yangu nilihisi yule mzee atakuwa mwanga tu.
Punde kidogo vijana wawili wakiwa wamevaa mashuka mmoja shuka jeusi na mwingine shuka jekundu walitokea mwelekeo ule ule aliotokea yule mzee wakiwa wanaongozana. Mmoja alikuwa amebeba mshumaa unaowaka na mwingine amebeba njiwa. Baada ya kufika karibu na mimi wa kwanza aliniuliza "Upo salama wewe?" sikumjibu chochote, nakumbuka nilikuwa natafuta tusi la kumpa lakini sikulipata kwa haraka, mdomo kila nikiufungua ulikuwa unanisaliti, nilibaki tu nayumba yumba huku nikichezesha mikono kana kwamba kuna kitu nataka kuongea lakini sikikumbuki, wakati nipo katikati ya hiyo hali basi yule kijana wa wa pili akaniuliza swali jingine""Shetani ameelekea wapi?" Sikuwa na jibu la haraka haraka kumpa maana nilifikiri amekosea kuuliza swali. Akauliza tena "Umemwona Shetani?" Safari hii nililisikia swali vizuri. Ikabidi niache kuyumba nikae kikakamavu kama vile askari kamwona mkuu wa kikosi.
Kwa sauti ya chini nikanyanyua kinywa nikawaambia "Sijamwona kwani vipi?" Ghafla bin vuu wakatimua mbio kila mmoja na mwelekeo wake aliyebeba mshumaa aliutupa chini na kuelekea alipo elekea yule mzee karibu na vichaka akapotea yule mwingine alirudi alipotokea akiwa amemshikilia yule njiwa pasipo kumwachia. Nilishikwa na butwaa nisijue nikimbilie wapi. Maana safari yangu ilikuwa imeingia mkosi. Kwa takribani sekunde tano hivi kichwa hakikufanya maamuzi yoyote ndipo niliamua kujipiga makofi mawili matakatifu pombe ipotee. Ile natafuta njia ya kukimbilia mara nikamuona yule mzee aliyenipita mara ya kwanza anatokea kichakani huku anakimbia.
Eee bwana eeh, nyuma yake kulikuwa na kundi la watu linamkimbiza.....
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kaazi kweli kweliMajira ya saa saba usiku nikiwa nimetoka bar akili ikiwa imeshachoka kutokana na balimi tisa nilizopiga nilikuwa nakatiza mtaa wa mkwajuni karibu na makaburi ya wahenga wa mtaa huo uliopo maeneo ya Tabata Kajiungeni. Ghafla nilikutana na mzee mmoja wa makamo aliyeniangalia usoni kwa kunikazia macho kana kwamba ananidai kisha hakuongea chochote zaidi tu ya kuguna na kutema mate chini kisha akanipa mgongo na kuchikichia kichakani. Kwa mawazo yangu nilihisi yule mzee atakuwa mwanga tu.