UKI nakubaliana na wewe. Ungeweika post yako kwenye paragraphs ingesomeka vizuri. Tatizo kubwa linalotukabili ni kwamba Watanzania tuna tabia ya kuyakimbia matatizo na kuongea kinafiki. Sioni tofauti iliyopo kati ya suala la muungano na suala la ushoga. Tunajua kabisa kuwa kuna masuala yanatakiwa kuwa addressed. Lakini tunayafumbia macho huku tukisema hakana tatizo.
Nakumbuka Waziri Membe alisema kuwa "Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje". Ukweli ni kwamba ushoga upo Tanzania, tena sana tuu. Japokuwa kuna tamaduni na sheria zinazopiga marufuku ushoga, hii sheria haijawahi kuwa enforeced ipasavyo. Watu wanajifanyia ushoga watakavyo.
Kama alivyowahi kuandika mwandishi mmoja "
Tatizo ni unafiki wetu, sio ushoga". Wapo mashoga wengi tuu maeneo mbalimbali ya Tanzania hasa Dar Es Salaam. Kuna "idadi kubwa tuu ya mashoga katika maeneo mbalimbali ya burudani jijini Dar es Salaam. Na uchunguzi usio rasmi ulionesha kuwapo kwa mashoga kwenye kitchen parties ni kama suala la kawaida tu….kumbi za muziki wa mwambao… ni chaguo kubwa la mashoga."
"Lakini jambo moja la wazi ni kwamba hakuna upinzani, chuki au hasira dhidi ya mashoga hao. Na sijawahi kusikia kuna shoga amekamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani na hatimaye kufungwa kwa "kosa" la kuwa shoga.":
http://www.raiamwema.co.tz/tatizo-ni-unafiki-wetu-si-ushoga
Kwa hiyo, nakubaliana na
Boflo. Tuache unafiki. Ushoga umeota mizizi katika jamii yetu. Aina mpya ya ushoga ni hii ya watu wazima na pesa zao lakini ni mashoga wanawahonga pesa vijana wadogo, ili hawa vijana wawale tigo hao wazee. Hii ipo sana Dar Es Salaam na vijana wengi wa kizazi kipya wameshaona ni dili.