kitoto wa vitoto
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 375
- 419
Mimi labda nikushauri kwenye uhalali wa shamba,ni kweli kabisa maeneo mengi makubwa mkoa wa Pwani yanamilikiwa na watu. Sasa iko hivi wamiliki waliwaweka watu wa kuyalinda,mlinzi anakaa hata Zaidi ya miaka kumi kwenye eneo anaingia tamaa kutokana na kila uchwao ugumu wa Maisha unaongezeka. Mnunuaji unaingia mkenge unanunua,mlinzi anakimbia balaa linabaki kwako. Hayo maeneo kuna watu wanayalipia kabisa,hivyo ni vizuri ukaingia hata Halmashauri ya eneo husika kusaka taarifa za eneo. Achana na majirani,mwenyekiti wengine ni wakufika tu au wamepewa Mlungula.Poleni na hongereni kwa pilika za maisha
Mm ni kijana wa umri wa kati pungufu ya 30
Nilikuwa na wazo la kilimo kwa siku nyingi na niliweka malengo kudunduliza mpaka nitimizehszma yangu
Hatimae nimefanikiwa kupata eneo mkoa wa pwani kata ya tarawanda (chalinze) eneo ni ukipanda na barabara ya kwa mwarabu kuna kijiji kidogo kipo karibu na shule ya msingi ndo maeneo hayo kwa ndani kidogo .
Lengo langu ni kufuga kisasa, kulima kisasa kuweka miradi midogo midogo pia
Je eneo hilo ni mali ya wananchi kweli au ni eneo la mwekezaji? (Kuna member mmoja alisema maeneo hayo kuna shamba la watu hivyo tuwe makini) nimewasiliana na viongozi kupitia watu wengine ila viongozi wamesema ni mali yake na ni halali
Naomba mnishauri
1 kuhusu uhalali au tahadhari ya maeneo hayo
2 hali ya hewa ya huko hasa mvua nk
Upatikanaji wa maji ya kuchimba
4 ushauri mwinginro.
Note
Shamba nimepata ila bado sijalilipia
Karibuni kwa ushauri na mapendekezo
Natanguliza shukrani
Asante kwa ushauri nduguKafuge nguruwe, miaka miwili tayari wewe ni mengi.
Asante sana mkuu nitafuatiliaMimi labda nikushauri kwenye uhalali wa shamba,ni kweli kabisa maeneo mengi makubwa mkoa wa Pwani yanamilikiwa na watu. Sasa iko hivi wamiliki waliwaweka watu wa kuyalinda,mlinzi anakaa hata Zaidi ya miaka kumi kwenye eneo anaingia tamaa kutokana na kila uchwao ugumu wa Maisha unaongezeka. Mnunuaji unaingia mkenge unanunua,mlinzi anakimbia balaa linabaki kwako. Hayo maeneo kuna watu wanayalipia kabisa,hivyo ni vizuri ukaingia hata Halmashauri ya eneo husika kusaka taarifa za eneo. Achana na majirani,mwenyekiti wengine ni wakufika tu au wamepewa Mlungula.
Samahani mkuu, coment ya kwanza nimeweka bila kusoma uzi wako.
Nyie ndiyo mnasababisha migogoro ya ardhi iendelee kuwepo.
Kuna sehemu umeandika eti "umewasiliana na viongozi kupitia watu wengine" hilo tayari ni tatizo.
Wanaweza wakawa ni viongozi kweli, uwezekano mkubwa upo pia wakawa ni matapeli weungana ungana humo humo mpaka wamepatikana viongozi.
Wewe ili kuthibitisha kwa uhakika zaidi, tenga japo hata siku kadhaa tofauti tofauti ndani ya mwezi, nenda huko unapotaka kununua eneo, ongea na wenyeji wa pale, ili kupata uhakika zaidi, usiende na muuzaji anayetaka kukuuzia, wewe nenda wewe kama wewe. Tena siyo mara moja.
Nimeandika hayo kwa kuona una wasi wasi (hofu) fanya hivyo kujiridhisha zaidi.
Kuna mtu alienda kununua kiwanja, huko anapoenda kununua kiwanja hakuna yeyote wanaye fahamiana naye.
Kufika kule wenyekiti vitongoji mpaka mabalozi wa nyumba kumi walikuwepo (kumbe wote hao ni matapeli, sema tu wamepeana vyeo wao kama wao) mwisho wa siku anakuja kuambiwa wale ni matpaeli hakuamini.