Ushauri: Tunza MSG za Miamala ya Fedha, Ningelala Selo leo

Ulicheza kama pele ila next time tumia app za pesa kama tigo pesa app au m pesa app zile zinatunza kumbukumbu za muda wote ukitaka miamala hata ya miezi kadhaa nyuma unaipata na unauwezo wa kuipata kupitia simu yoyote ukiingiza id yako tu ya pesa husika
 
Hata kama ungefuta hizo meseji ungesumbuka tu kukaa polisi na ukapata dhamana. Upelelezi ungeonyesha pesa alipokea. Hata kesi ingepelekwa mahakamani ungeshinda asubuhi tu. Kilichokusaidia ni kuepuka usumbufu tu.
Pesa ya kupewa ambayo unaweza kuikana ni ile ya mkono kwa mkono tu na si vinginevyo. Ukitaka kumpa pesa mtu ambae unahisi atakukana mtumie kwa njia ya benki au kwenye simu hata ikiwezekana mtumie na ya kutolea akitaka.
 
Niliwahi kumuwekea jamaa muamala akaondoka akakaa baada ya siku Tatu akarudi tena eti pesa haijafika nioneshe ushahidi..nikamuuliza inakuwaje ukae siku mbili mzima bila ya kuiona pesa na usirudi!!! Akaleta mbambamba nyingi! Nikamuonesha meseji akatoka na aibu!! Mwafrika ni mtu wa hovyo!
 
Asante kwa taarifa
 
Kwa sisi watumiaji wa viswaswadu tunatunazaje miamala hasa hii ya wateja wa Kila siku?
 
Mkuu upo kijiji gani huko wasiojua miamala unaweza kuomba statement kutoka mtandao husika na wakakutumia within a minute?

Au huyo demu nati zimefunguka sasa utapeli gani huo wa kifala...
 
Pole sana mwamba
 
Mbona unaweza kupata statement kama za bank tu.
 
Yani usifute meseji wakati application za mitandao ya simu unaweza kuvuta statement ya miamala yako yote
 
Mi huwa naomba statement kwa network provider wanantumia kwenye email ko naweza kuprint au nikaiacha kama ilivyo soft copy

Jitahidi sana malipo yo yote yale yapite kwenye transection ili kuepuka watu wasio waungwana au ikiwezekana malipo yawe kwenye maandishi kumbuka kuandika tarehe muda na umsainishe kama yupo karibu na notebook

Binadam haaminiki wala hatabiriki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…