Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia juu ya muonekano hasa mavazi ya walinzi wa chadema ,hakika kuna kasoro kubwa sana, japo sisi kama wapenzi wa mabadiliko hatujaliona hili, lakini ni hatari kwa siasa zetu. Mavazi wanayovaa hayana tofati na majambazi au wezi kwa muonekano halisi. Unakuta mtu kavaa vya ajabu hadi anatisha hujui huyu ni bodaboda ,mlinzi au kibaka . Chadema naamini tunaweza kuwawekea walinzi wetu style nzuri ya mavazi ambayo ni ya kistaarabu na kuwafunza kuvaa smart hasa matumizi ya miwani ,kwani yana mahali pake sio kila sehemu ni miwani tu.
Napenda sana aina ya mavazi ya makamanda hawa tena nasema wasilegeze kamba na kama ingekuwa inawezekana wangeongezewa mafunzo ikiwezekana hata nje na wawe wanalipwa posho nzuri