Ushauri kwa wale waliooa tu

mtoto wa maskini

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
1,152
Reaction score
638
Wadau mimi ni kijana nimeoa miaka 2 iliyopita lakini kipindi hiki cha mwaka mmoja wife yupo mbali na mimi na kuna uwezekano akakaa zaidi ya mwaka kulingana na kazi zake anazofanya na mimi makazi yangu yapo mbeya, miaka yote hii miwili nimevumilia sana kuchepuka na kweli nimefanikiwa ila sasa ivi nimekuwa na hamu ghafla ya tendo la ndoa na kibaya zaidi nimejaribu kupiga masterbation kutuliza lakini haisaidii ninaenda gym bado haisaidii, kwa wale wenye uzoefu na kukaa mbali na wake zao na wasichepuke naomba ushauri mana naisi nitachepuka hali ikiendelea ivi kiti ambacho sipendi kitokeee
 
Ngoja tuanzie hapa kwnza, kwani huo mwaka moja ulikuwa unafanyaje brother mpk ukafanikiwa kumshinda adui shetani
 
thatha wewe kaaga na maugwadu yako hivo hivo wakati mwenzio anahuzuria ibada kila wiki! 😕
 
Acha ujinga. Uliona wapi mume akae Arusha na mke akae Songea tena miaka kwa kisingizio cha kazi. Haya endelea na huo ujinga.
 
ukitaka kuvishinda ivyo vishawishi fanya sana ibada then kuwa karibu na allah
 
Kazi gani hizo za kukaa mbali miaka miwili bado muwe mke na mume? mtoto akizaliwa hapo kuna asilimia kubwa kuwa sio wako fanya utaratibu haraka umuhamishe huko aliko lasivyo utajikuta wewe unajibana yeye anajiachia
 
Kazi gani hizo za kukaa mbali miaka miwili bado muwe mke na mume? mtoto akizaliwa hapo kuna asilimia kubwa kuwa sio wako fanya utaratibu haraka umuhamishe huko aliko lasivyo utajikuta wewe unajibana yeye anajiachia

Yeye ni mchumi anafanya kazi halmashauri moja kanda ya ziwa na sasa ivi ni kudumu yani ndo kituo chake cha kazi mimi nipo taasisi ya serikali pia hapa mbeya, kuhama nilijaribu mwanzoni ila ikashindikana
 
Utamuua mwenzio kwa presha ohooo

Afe tu kwani amewesa kufumilia mwaka wakati mwenzie wiki tu yamshinda.

I bet dogo hayuko sirias na ata mke hana. maelezo yake yanacredibility ndogo sana.
 
Hee!? Kwahiyo hata likizo hampati kwani nyie si watumishi wa umma.
 
Yeye ni mchumi anafanya kazi halmashauri moja kanda ya ziwa na sasa ivi ni kudumu yani ndo kituo chake cha kazi mimi nipo taasisi ya serikali pia hapa mbeya, kuhama nilijaribu mwanzoni ila ikashindikana

Fanya juhudi umuhamishe mkuu la sivyo hiyo sio ndoa nakuambia ukweli, mwanamke huwa anafananishwa na mtoto kimtazamo kwa maana ya kwamba mtoto akiwa karibu na wazazi anakuwa katika misingi na msimamo wa wazazi wake,

Na kamwe hawezi kwenda nje ya hapo hata akiwa mkubwa utaona mfumo wa maisha yake unafuata msingi wa wazazi wake vivyo hivyo kwa mke akiwa karibu na mumewe ataishi kulingana na msimamo wa mume hata akibaki peke yake ataishi kwa mfumo huo sasa wewe wa kwako hana mfumo wala msimamo wako kwa sababu ndoa yako ina muda wa miaka miwili na hiyo yote mnaishi mbali mbali, atakopi tabia za wanaume wengne.

mwisho wa siku atakuona wewe haumfai, na kumbuka msimamo wa wanawake juu ya mumewe huimarika pale anapokuwa na mume wake karibu maana mume anakuwa kinga yake hata watakapokuja wengine kumtongoza atasimama kwa kinga ya mume wake.

Sasa wako ni ngumu anaweza akaweka msimamo lakini wapo wanaume vichwa ngumu watamshawishi mwisho atakubali huku akijipa moyo uko mbali anafanya kidogo tu, ni wako tena huyo? na hapo wanaume hufanya jitihada za kumteka kabisa watu watazama chumvini hata siku za MP utakuja unalia hapa, fanya mpango hakuna linaloshindikana ukilivalia njuga otherwise unataka tukupe ruhusa ya kuchepuka.
 
Hapo Mwanamke Kumuachisha Kazi Ili Awajibike Kwenye Wajibu Wake
 
Ngumu kumesa....lakini hakikisha unamfata au anakufata...kwani umeshakata tamaa ya kutafuta uamisho.
Me mjinga anaalibu ndoa yake ye mwenyewe...and vice versa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…