Naomba nianze kwa kusema hakuna aliyemkamilifu chini ya jua na siku zote mtu mwenye hekima anapotambua mwenyewe kuwa amekosea au kuonyeshwa na mtu mwingine kosa hujirekebisha na kisha kusonga mbele. Wabunge wangu wa CHADEMA inaonekana ninyi ndio hamtumii vizuri kanuni za Bunge.Tunafahamu kuna propaganda za wabunge wa CCM zinazorushwa kwenu na saa nyingine lugha za maudhi lakini mimi binafsi nawaomba na kuwashauri mtumie vizuri kanuni za bunge na mahali inastahili kutumika mnapotaka kujibu hoja za wenzenu wa CCM.Kwa mfano ktk kikao cha leo Mbunge wa Iringa mjini alionekana kutumia kanuni isivyo alipokuwa akitoa taarifa yake (badala ya kutumia kanuni ya kutoa taarifa alitoa kanuni ya kuomba mwongozo).Tunaomba msifanye vitu ambavyo vitawaondolea heshima yenu kwa wananchi ambao wanawaamini. Pia nafahamu mna kuna mambo ya kuwaudhi humo bungeni wakati vikao vinapokuwa vinaendelea kama kejeli na mambo mengine mengi na saa hamuwezi kukaa kimya na ni vizuri kuwajibu, binafsi nawashauri mjikite kwenye mambo ya kuwatetea wananchi na mambo yanayoleta maendeleo kwa taifa letu. Mwisho nawatakia kazi njema mnayoifanya hapo bungeni.

kwa hali iliyosasa hata Spika anasema anatumia kanuni za Bunge Lakini ukweli ni huu kuwa hata mtu yeyote anajua kuwa kuna upedeleo wa wazi kuhusu utendaji wa spika na Wenyeviti wake.
Mbunge wa Sikonge alisema kuwa " mwenye uchungu akazae" aliyasema haya huku akichangia bajeti kila mytu anajua mbunge huyu hakuwa anachangia suala la Afya lakini Naibu Spika akasema si tusi wala si kosa.
Jana Mwenyekiti anapombwa mwongozo kwa kanuni yeye anatoa mwongozo kuwa Tundu Lisu anataka umaarufu
Baadaye anamtukana Mnyika kuwa "anawashwa" huyu ni mtu anayeonekana kuwa mzee wa kuaminika ndani ya CCM na kwa taifa anatumia misemo ya mateja mitaani.
Wabunge wetu endeleeni kusimamia hoja mjikaze ili kuepusha hasira katika haya mazingira WANANCHI TUNAONA,TUNASIKIA,TUNAJUA na sasa tumeshatoa hukumu ambayo munaiona katika mikutano yenu kwa imani inayooneshwa na WANANCHI juu yenu.