Ushauri kwa UKAWA

donniebrasco

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
887
Reaction score
775
Habari ndugu zangu,

Viongozi wa upinzani nawashauri kuwa mnakaa pamoja mara kwa mara kujadili mambo mbalimbali ambayo mnaona yana umuhimu katika kuishauri serikali au jamii kwa ujumla na kisha baada ya hapo mnakubaliana kwa pamoja ikiwezekana hata kwa maandishi na kuwe na msemaji mmoja rasmi ambaye yeye ndo atakuwa anaongea na serikali, vyombo vya habari au na walengwa wengine.

Nilikuwa naamini huu utaratibu mnao lakini kidogo kwa siku za karibuni nimeona mkisema mmoja mmoja.

Najua mnayo haki ya kusema mmoja mmoja na ninaheshimu haki yenu hiyo lakini naamini mkiweka utaratibu huo ( inawezekana upo au ulikuwepo kwa hivyo ufuatwe)

Hii tabia ya kila mmoja kuwa anakurupuka na ya kwake itawapunguzia heshima na pia ni rahisi kwa mmoja mmoja kufanya makosa katika uwasilishaji au hata katika kujenga hoja na hivyo kupelekea kutotiliiwa maanani kwa maoni mbalimbali

Na pia inaweza kuleta dhana mko zaidi katika kutafuta "kick" binafsi.

Asanteni sana.
 
Siasa hadi 2020 isipokuwa kwa sizonje na chama chake. Tinajenga vwonder kwa mwendo kasi kwa matrillion ya accasia. Subiri Noah yako
 
ni kweli mkuu ni lazima atleast waonekane kwenye media tusiwasahau 2020,lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…