Ndugu wana Jamii Forum,
Kwa mara nyingine tene nasikitishwa na kufungwa kwa timu yetu ya mpira wa miguu ta Taifa Stars na Amavumbi!
Hivi sisi tutakuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka lini? Tangu Mzee ruksa atoe msemo huo ni takriban miaka 20 sasa, bado tuu, twanyolewa tuu, du kazi kweli kweli!. Nangoja mechi na Brazi sasal!!
Mimi naona mfumo mzima wa michezo TZ ufumuliwe turudi enzi za baba wa Taifa ambapo tuliweza kuzalisha wachezaji chipukizi kama akina Niko Njohole, Rahim Lumelezi, Martin Kikwa, Sunday Manara, Kibadeni; mabondia kama Aloyce Nutti, Emmanuel Mlundwa, Isangura; wakimbiaji kama Nzaeli kyomo, Mosi Ali, Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, nk. Wachezaji wengi walipikwa mashuleni, na makocha wa kitanzania!!!!. Hatukuwa na akina Marcio Maximo. Mfumo wetu wa elimu ulitambua mahusiano kati ya michezo na elimu na serikali ikawekeza katika michezo. Wakati huo hatukuwa na facilities na rasilimali mali na watu kama tulizonazo sasa, ila tulikuwa na utashi wa kisiasa kwa viongozi wa serikalini wa michezo,na uwajibikaji wa hali ya juu kwa viongozi wa michezo kama Mzee Saidi El Maamry, na kwa wachezaji pia. Viongozi wa michezo na wachezaji walitanguliza zaidi maslahi ya Taifa kuliko ubinafsi wa kutafuta mianya ya rushwa ndani ya michezo. Sasa hivi tuna resources na access ya mpaka ligu kuu duniani kama vile Premier League, Bundersliga, French Premier League, Spanish league, olympics nk. Enzi hizo kwa sisi tuliokuwa tunafuatilika mpira nyumbani ni RTD tuu, saa mbili kasoro robo usiku au mpira utangazwe live, tuwasikie akina Abdul Omary Masudi, Ahmed Jongo, n.k na walituhamasisha kwelikweli, tukahamasika, na wachezaji wakafanya kweli.
Sasa hivi michezo imekuwa ngazi ya kupandia katika ulingo wa siasa na porojo kabakaba. Kila waziri wa michezo na/au wa elimu anakuja na sera tofauti na zinazokingana na maslahi ya wananchi katika michezo. Tukishindwa kuruzisha michezo enzi za Mwalimu basi tuangalie alternative ya ku- out source kwa wawekezaji wa nje wizara ya michezo na uongozi wa vyama mbalimbali vya michezo vinavyozalisha watalii badala ya kuzalisha wachezaji. Food for Thought.
Regards,
JMU