Ushauri Katika Kukuza Vipaji Michezoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri Katika Kukuza Vipaji Michezoni

Discussion in 'Sports' started by TingTing, Jun 3, 2010.

 1. TingTing

  TingTing Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikijaribu kuangalia ni namna gani ambavyo nchi kama Tanzania inaweza kuza vipaji vya wanamichezo hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi sekondari ili kulinyayua Taifa kimichezo na angalu kujiweka katika ramani ya michezo duniani.


  Nimegundua kuwa kuna njia nyingi za kuweza kufanikisha hili suala na pia kuna njia mbadala za kuweza kugundua vipaji vya wanamichezo na kusaidia kuvikuza. Ila hapa nimeona nishauri njia moja ambayo wengi wetu huwa hatuitilii maanani ambayo ni ile ya wale wanamichezo ambao tayari wako katika nafasi ambazo wanaweza saidia wengine kuonekana ila wanapuuzia kabisa. Ukiangalia nchi kama Nigeria, Cameroon, Ghana, Senegal na Mali tangu zamani au Kenya wanavyofanya sasa hivi ni kuwa wale walioko nje ya nchi wakichezea timu tofauti tofauti wanafanya kila mbinu na njia kuwaunganisha wenzio waliopo nyumbani kwenye timu za huko nchi waliko. Hii imefanya vipaji kunyanyuka kwa haraka sana na leo hii tunaona ya kuwa kuna wachezaji wengi wanaocheza nje ya Kenya, nje ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Ben Iroha, Stephen Keshi, Sunday Oliseh, Daniel Amokachi, Austin JayJay Okocha, Finidi George, Yekini, Kanu, Victor Ikpeba, Amunike, Tijani Babangida, Samson Siasia, Mutiu Adepoju n.k.


  Pendekezo langu kubwa hapa ni kwa wanamichezo kama Hasheem Thabit, Henry Joseph na wengineo wengi tu ambao wako katika timu tofauti tofauti na michezo tofauti tofauti duniani wajaribu kuwaunganisha wachezaji ambao wanaonekana na kiwango kizuri cha kucheza mchezo husika. Kikubwa sio wachezaji wa ligi kuu, hapa sanasana ni wale wanaochipukia katika shule za sekondari. Vilevile hii si tu kwa wanamichezo pekee bali hata kwa wazawa walio nchi tofauti nje ya Tanzania, tukiwa na lengo la kusaidia taifa katika dira ya michezo.


  Kama kuna mtu anajua mchezaji mpira au kikapu mzuri katika shule za sekondari haswa wale walio kidato cha tatu na kuendelea tafadhali asisite kunigota. Kwa kumalizia napenda kusema kuwa mie nitajitahidi kuwaunganisha na wadau mbali mbali pamoja na watu wangu wa karibu ndani na nje ya nchi pia kama itawezekana. Na hapa inabidi tuondoe fikra potofu za "HAKIWEZEKANIKI" hii ndio inatuangusha sie sana. Binafsi naamini kuwa kila kitu kinawezekana iwapo subira hipo na tumejitolea kikamilifu kufikia malengo yetu. Watanzania tusaidie kuinua michezo katika nchi yetu, hakuna wa kutufanyia ni sis wenyewe kwa kusaidiana ndio tunaweza kufika walipo fika Ghana, Senegal, Cameroon, Mali, Nigeria na nyinginezo nyingi tu.
   
 2. J

  JMU Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana Jamii Forum,

  Kwa mara nyingine tene nasikitishwa na kufungwa kwa timu yetu ya mpira wa miguu ta Taifa Stars na Amavumbi!


  Hivi sisi tutakuwa kichwa cha mwendawazimu mpaka lini? Tangu Mzee ruksa atoe msemo huo ni takriban miaka 20 sasa, bado tuu, twanyolewa tuu, du kazi kweli kweli!. Nangoja mechi na Brazi sasal!!  Mimi naona mfumo mzima wa michezo TZ ufumuliwe turudi enzi za baba wa Taifa ambapo tuliweza kuzalisha wachezaji chipukizi kama akina Niko Njohole, Rahim Lumelezi, Martin Kikwa, Sunday Manara, Kibadeni; mabondia kama Aloyce Nutti, Emmanuel Mlundwa, Isangura; wakimbiaji kama Nzaeli kyomo, Mosi Ali, Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, nk. Wachezaji wengi walipikwa mashuleni, na makocha wa kitanzania!!!!. Hatukuwa na akina Marcio Maximo. Mfumo wetu wa elimu ulitambua mahusiano kati ya michezo na elimu na serikali ikawekeza katika michezo. Wakati huo hatukuwa na facilities na rasilimali mali na watu kama tulizonazo sasa, ila tulikuwa na utashi wa kisiasa kwa viongozi wa serikalini wa michezo,na uwajibikaji wa hali ya juu kwa viongozi wa michezo kama Mzee Saidi El Maamry, na kwa wachezaji pia. Viongozi wa michezo na wachezaji walitanguliza zaidi maslahi ya Taifa kuliko ubinafsi wa kutafuta mianya ya rushwa ndani ya michezo. Sasa hivi tuna resources na access ya mpaka ligu kuu duniani kama vile Premier League, Bundersliga, French Premier League, Spanish league, olympics nk. Enzi hizo kwa sisi tuliokuwa tunafuatilika mpira nyumbani ni RTD tuu, saa mbili kasoro robo usiku au mpira utangazwe live, tuwasikie akina Abdul Omary Masudi, Ahmed Jongo, n.k na walituhamasisha kwelikweli, tukahamasika, na wachezaji wakafanya kweli.

  Sasa hivi michezo imekuwa ngazi ya kupandia katika ulingo wa siasa na porojo kabakaba. Kila waziri wa michezo na/au wa elimu anakuja na sera tofauti na zinazokingana na maslahi ya wananchi katika michezo. Tukishindwa kuruzisha michezo enzi za Mwalimu basi tuangalie alternative ya ku- out source kwa wawekezaji wa nje wizara ya michezo na uongozi wa vyama mbalimbali vya michezo vinavyozalisha watalii badala ya kuzalisha wachezaji. Food for Thought.

  Regards,

  JMU
   
Loading...