Ushauri juu ya ving'amuzi

REMSA

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
2,579
Reaction score
956
Nadhani mpaka kufikia leo tarehe 08/01 wengi mmeshatumia ving'amuzi na
tayari mnajua King'amuzi kipi bora,sasa naomba ushuri wenu ninunue King'amuzi
kipi"
 
hadi sasa sokoni kuna ving'muzi kama ting,startimes,easy tv,na zuku.ila zuku na easy tv ni vya kulipia zaidi tofauti na ting na startimes.nadhani hadi sasa kidogo cha startimes ni bora zaidi japo inategemea na mahali ulipo kwani hata hapa dar tu kuna baadhi ya maeneo kinasumbua mala picha zisimame simame,kwa upande wa ting kuhusu muonekano uko poa sana ila tatizo lao kubwa ni package yao haina chanel nzuri,ila za hapa tz zote zipo ila za nje ni ovyo tu nyingi ni zile ft(free 2 air)chanel nzuri waliyo nayo ni ile emanuel tv,ambayo watu wengi sana wanaipenda,hata startimes ilikuwepo na baada ya kuitoa watu walilalamika sana!ngoja tusubili hivyo vya btl na continental vitangavyoingia sokoni hivi karibuni,kifupi hadi sasa bado ni MAGUMASHI MAGUMASHI TU.
 

Asante mkuu kwa ushauri wako"
 
Kilicho bora ni Dstv kikifuatiwa na Zuku ,wengine kumfuko ndio kunachagua king'amuzi cha kununua , wengi wamekimbilia king'amuzi cha Fastjet(StarTime)sababu ya unafuu wake na si ubora wake,ni sawa na ule usemi kwenye elimu ''Bora Elimu na si Elimu Bora''
 

Asante"
 

Mkuu ubaya wa hizo ulizozitaja nikuwa local chanel ni moja tuu TBC!
MAGUMASHI YANAENDELEA1
 

Ni sawa kabisa "Denis the manace"!

DSTV ni bora kwa ving'amuzi, hasa kwa digital transmission, kuna HD pale, ambayo kama utaelezwa jins ya kuitumia basi utafaidi sana, ila tatizo ni hio bei na kwa DSTV kutokuweka terrestrial channel, yaani channel za kawaida.

Ukitaka ubora DSTV Star Times na vinginevyo, huu mfumo utatupeleka mbali (wa digital) labda tutafika wakati tutakua tunasoma habari za kitaifa, dunia, technology, afya, siasa, udaku, michezo, timetable za ndege, matangazo na entertainments n.k. kupitia mfumo huu, hapa JK na serikali yake niko naye 110%
 
DSTV inaendelea kuridhisha na kuonyesha dhamani halisi ya pesa japo sio mpenzi na siangaliagi TBC sasa hivi mara moja moja nachungulia nikikuta vipindi vyao vya kigamba gamba narudi 203 na 207 najua wenye DSTV wanaelewa au 200 kupata taarifa kama nimelipia ile ya bei zetu,so nasonga mpaka kingamuzi cha uhakika kije ila kwa sasa nakushauri DSTV tena AfCON inaanza 19 mwezi huu nshasahau Isdingo the need mimi ila inaniuma.
 

Mkuu nieleweshe HD ni nini binafsi sijui kuitumia mwaka wa nne huu na DSTV leo ndio nasikia HD,tafadhali nijuze na mimi niifaidi
 
Mkuu nieleweshe HD ni nini binafsi sijui kuitumia mwaka wa nne huu na DSTV leo ndio nasikia HD,tafadhali nijuze na mimi niifaidi

HD au High Definition in digital transmissiom ni mfumo mpya kidogo huku kwetu, wenzetu walianza nayo muda kidogo, picha inakua clear mno, sauti toka kwenye picha iko nzuri au stereo au dolby zaidi, inaweza kurekodi vipindi, ku fwd au rwd, kuna memory pale ya kukuwezesha kuhifadhi vipindi vijavyo, mpaka kwa wiki kama ukitaka, una set tu kuanzia muda unaotaka na basi vinakuja ukifika muda, ni nzuri hasa sie wenye watoto wanaopenda tazama vpindi vyao, basi wewe unaset au ku record, na ukipata muda unatazama, kunakua na ka memory fulani ili kuweza kuhifadhi hivi vipindi, wenyewe watakueleza zaidi, ina maana wakati unatazama kipindi chako chochote, unaweza kuweka pause, ukachemsha chai na kujiwekea kahawa na kashata n.k., ukirudi una press play kama dvd unaeendelea, na hapo hapo unaweza ku fwd kama kama unataka.
Nawalaumu DSTV kwa kiasi fulani kwa kutokutangaza hii huduma muhimu kwa ufanisi zaidi.
Ila kama una pesa yako, mkuu chukua...
 
kanunue dish utapata chanel bure kama alivosema richard mlangi hapo chini
 
Mkuu ubaya wa hizo ulizozitaja nikuwa local chanel ni moja tuu TBC!
MAGUMASHI YANAENDELEA1
Unakijua unachokisema lakini?,kwa Dstv ni sawa lakini Zuku wana TBC,Channel Ten na Clouds.Tena Zuku na Dstv utawapata hata ukiwa Ngara au Liwale kwa kuwa wanatumia setalaiti ,sasa StarTime mpaka antenna iangalie Kisarawe,na je mkazi wa Liwale au Ngara naye aelekeze antenna Kisarawe?Pia Zuku wana radio stations kibao,
 
Hawa watu wa ving'amuzi magumashi tupu.Iweje channel za free to air watulipishe?Mfano startimes channel kama BBC,Al Jazeera,TBN,CCTV na nyingine za nje ni channel za free to air.iweje watulipishe pesa.Dish mpango mzima.Faida ya dish hakuna kulipia vilevile unaweza kuongeza na kupunguza channel.
 
mkuu hizo ndo tosha kwako!?
TBccm
Cluodsccm
channel ten hawaeleweki
MAGUMASHI MKUUU!
 
Mpaka hapa nyota tupu" huuuu niko hoi,bado sijapata uhakika wa king'amuzi kitakachoniwezesha
kuona hasa local channels nyingi kama si zote"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…