Nyerere aliwahi kusema 'CCM si baba yake wala mama yake' unaweza kuazima maneno hayo na kuyafanyia kazi.
Pamoja na juzi Mahakama kuonekana inaku favor lkn ujue haiko upande wako, kifupi wanakupotezea muda bure.
Umejionea leo, pamoja na Mahakama kuweka zuio la Mkutano Mkuu wamekaidi mkutano umefanyika. Ni juzi tu ulipeleka RITA majina ya Bodi yako imekataliwa ya Lipumba imesajiliwa. Unasubiri ishara gani nyingine uamini.
Baada ya mkutano huu kinachokwenda kufanyika ni kukuvua uanachama, najua utakimbilia mahakamani but won't help anything.
Tunajua wewe una watu (wanachama) Lipumba and vyombo vya dola yaani Msajili, polisi na mahakama ni ngumu sana kumshinda kwa vile yuko planted.
You got two options to make, one, deflect to another new opposition party preferably CHADEMA, the earlier the better or you have to Resign politics, the choice is yours.
Ila usikurupuke, kabla ya kutangaza kuhama, andaa matawi yote na mashina ya CUF yaliyo loyal kwako bara na visiwani, siku moja muamue kufanya surprise mtangaze kuhamia CHADEMA, nakuhakikishia siku hiyo hata CCM hawatamani ifike.
Ijenge Chadema mpya hasa visiwani then gombea urais visiwani kwa tiketi ya Chadema you won't regret, Otherwise, labda kama umeamua kufia mahakamani.