Ushauri: Bustani ya Miti ya Matunda katika Nyumba

n
 
Habar yako Mangosteen na Malayapple ntazipata wp kwa Dar karibu na maeneo ya kigamboni
 
Update mkuu
 
Machungwa3
 
Ng'ombe wa Maziwa usisahau!
 
Nimshukurubaliyeanzisha huu Uzi, nilichukua hii idea na kuifanyia kazi mwaka 2016, kwasasa nyumbani kwangu Kuna matunda yafuatayo ambayo yameshaanza kuzaa Toka mwaka 2022
1. Mipera 2
2. Chungwa 3
3. Chenza 2
3. Miembe 6
4. Komamanga 4
5. Stakafeli 2
6. Zaituni 1
7. Parachichi 2
8. Papai 3
9. Tunda Damu 2
10. Passion 2
11. Kuna tunda lisijui jina 1
12. Pilipili 2
Nb. Niliongezea na miti 2 ya kivuli.
Kwa Sasa Nina matunda mengi nyumbani kwangu, tunatumia pamoja na familia bila kusahau majirani
 
Weka picha mkuu.
 
Reactions: Lax
Mimi pia mdau wa huu uzi, mwaka siukumbuki vizuri. Niliweka miembe kama 5, michungwa, mlimao mmoja, Mistafeli 3, Komamanga, Mipapai(Nililinunua Mbegu za kisasa), Mlonge, passion

Matokeo
Muembe mmoja uliwahi sana kuzaa maembe yasiyo na ladha(Baadae ukawa balaa maembe mengi matamu, miembe iliyobaki sio sana hadi leo.

Michungwa sijui changamoto yake, ilichelewa ila mmoja ulitoboa na uko vizuri sana. Mingine niliikata baadae mingine ikaota upya ikawa milimao. Michenza pia sikutoboa. Malimao ni mengi sana nyumbani mengine nasambazia upendo majirani na marafiki. Michenza pia sikutoboa

Mastafeli ni failure kuu, yanazaa ila yanaozea mtini yote.

Mapapai lilikuwa pakti zima, kama minne nilipanda sehemu nilikuwa namwaga mbolea zamani. Ilizaa mpaka mtu wa sokoni akaja kununua. Hii ilishakufa yote.

Komamanga nashindwa kuelewa, au labda mti unazaa matunda mabovu 😀

Mlonge pia changamoto, mti unakuwa mkubwa sana na sijawahi kutumia. Jirani mmoja alikuja sana kuchuma, kahama upo tu. Niliuchimba, vipande vilivyodondoka ukaota upya.

Topetope yalishika na kuzaa

Pilipili zilizaa sana ila haudumu, yalishakufaga

Mpera, kuna kipindi ulizaa mapera makubwa sana ila pia yanaharibikia mtini, ukiyawahisha yanakuja kuharibikia ndani

Minazi mifupi/madafu hapa nilijaribu mara nyingi ila sijawahi toboa, yote hufa mpaka nikanyoosha mikono pamoja na ardhi kuwa kichanga.

Passion pia safi

Nna mashamba nje ya mji, nataka kufanya hii kazi upya huko mashambani. Moja nna mpango wa kufanya makazi uzeeni huko. Nilikuta lina madafu tayari yaliyonishinda kupanda na matamu balaa, nitamalizia vilivyobaki. Miche nitaagiza kabisa Morogoro.

Mwisho nna swali, hivi maparachichi Dar yanatoboa vizuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…