Habari wakuu,
Hembu wazoefu wa kilimo,nipeni ushauri huu.
-Je mazao hayo yanaweza kuwa pamoja
-Kwa wazoefu,ni ukubwa gani wa eneo natakiwa niwe nao kwa miti yote hiyo.Just for trees tu,maana ukubwa wa House,swimming pool,tennis Court(converted to Basketball pitch and Volleyball pitch) ukubwa wake ninao tayari.
-Ushauri mwingine wa ziada pia unakaribishwa
List hapa chini ila mwenye ziada anaweza kuongeza
Aina ya mti na idadi yake
1)Miembe 2
2)Mipera 2
3)Avocado 1
4)Michungwa 2
5)Michenza 2
6)Ndimu(Lime) 2
7)Lemon 1
8)Komamanga 2
9)Shokishoki(Rambutan) 2
10)Minazi 6
11)Michikichi 4
12)Apples 6
13)Stafeli 3
14)Bilimbi(mbilimbi) 2
15)Topetope(Custard Fruit) 2
16)Carambola 2
17)Minanasi 10
Ziada nimeyopata kwa mdau humu
Chaula Rich
Naongeza
18)Fenesi(Jack Fruit) 1
Ziada ya mdau
chuma cha rel
19)Bungo Tree 2
20)Mipapai 6
Ziada ya mdau
Rolandi
21: Pilipili,miti 10 au 20 ya aina tofauti
Ziada kwa mdau
Kingmairo
22:Zambarau 1
Miti tiba:
Karafuu 2
Mironge 2
Hiyo ni idea nzuri. Mimi kwangu nimefanya hivyo, nimepanda aina nyingi ya miti ya matunda na sasa yana mwaka wa pili hivi. Mingine tayari imeanza kuzaa (mipapai, mipera, carambola).
Ila ningekushauri miti ifuatayo uwe na hadhari:
-Michikichi ni ya nini kwenye yard? Ikiwa utapenda labda panda mmoja au miwili tu.
-Apples haziwezi kuota kwenye joto, zinahitaji kipindi cha baridi katika ukuaji wake, sawasawa na peaches na plums (matunda damu)
-mishoki shoki hebu cheki nadhani unahitaji mitatu (ulizia kama iko dume na jike tafauti.... ni vyema ukaenda kituo cha utafiti kizimbani kupata usahihi zaidi). Pia upate aina ya 'nyama peke yake' - ulizia kwa wenye mishoki shoki aina hii maeneo ya Mwera.
-mangosteen (ulizia kizimbani) matunda yake ni safi sana.
-miembe panda ile midogo ya kisasa.
-mitufaa (malay apples) iko mekundu na meupe. Ni mizuri kuipanda karibu na nyumba
-minazi chukuwa kitamli (ya madafu) ndiyoo mizuri karibu na nyumba. Ile mirefu (east african tall) yana changamoto zake, kwani nazi ikidondoka kutoka juu ni hatari.
- mzambarau, mkunazi au mkwaju kwa nyumba ya kawaida inakuwa mikubwa sana, labda kama utakuwa na shamba.
Ingependeza zaidi ukiacha sehemu ndogo kwa ajili ya kupanda mazao ya bustani - mchicha, matembere, nyanya, pilipili na vyengine vya msimu
Kuhusu spacing kwa miti aina ya mifenesi, miparachichi unatakiwa angalau iwe mita 5 x 5, na itapendeza zaidi ikiwa utapanda kwa mistari.