:help: Nashukuru Mkuu kwa msaada wako, lakin inaniwia ngumu kukumbuka vitu vyote nilivyotumia kwan ni muda mrefu tang nimeathirika na tatizo hili. Nina miaka mitano na unajua reception inapokua mbaya unahangaika kuiweka sawa, mara huyu anakuambia jaribu hiki. so nimepitia ving na sina kumbu kumbu ila baadhi kama. Mara nyingi nanunua farmasi vichub nakutajia ninavyovikumbuka sonaderm cream, safi cream, persol Gel 5.0, Gold tach cream, Malaika kutoka USA, na vingine ving ambavyo hata majina siyakumbuki. Si unajua unaweza kununua halafu unapaka ukiona hakuna mafanikio unaacha, unajaribu tana kingine ukiona hakifai unaacha. Mwisho ndo nimeenda kwa docta nikihisi mybe ni aleji kwa sababu kwa nini nikiingia katika hedhi zinakolea, wakati mwingine zinaisha halafu zinarudi tena.
nitashukur kwa msaada utakaonipa.
Natanguliza shukran zang za dhati