Ushamba wa PhDs na hatma ya nchi yetu

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,208
Elimu ni jambo njema sana. Linamfanya mtu kufungua ubongo wake kwa mapana.
Hata hivyo elimu tu haitoshi linapokuja suala la uongozi. Katika qualities za uongozi bora elimu ya madegree na maPhDs sio sifa namba moja.

Ni kama magadi tu lakini sio chumvi kwenye mboga tunayoita hapa kwa jina la 'uongozi'.
Uongozi unataka mtu mwenye busara, uvumilivu, subira, maono, hekima, msimamo thabiti na heshima kwa wale anaowaongoza. Vitu hivi si lazima uvipate darasani.
Daktari lazima asomee udaktari ili afanye kazi ya udaktari. Vivyo hivyo kwa mwalimu, mhasibu, lawyer, mhandisi nk.

Vilevile katibu mkuu wa wizara lazima awe graduate. Sawa. Hata hivyo kusoma pekee na kujaza mavyeti hakumfanyi mtu kuwa waziri mzuri. Si lazima sana waziri kuwa na elimu ya juu sana kuwa waziri mzuri kwani yeye ni mwanasiasa tu na hategemewi kuingia 'jikoni'
Elimu pia haimfanyi mtu kuwa mbunge mzuri. Mara nyingine hekima na busara tu zinatosha katika uongozi wa siasa.

Hivi sasa umeingia 'ushamba' wa kudhani kuwa viongozi wenye PhD ndio hamira ya maendeleo nchini.

Historia ya karibuni inatuonesha kuwa kuna viongozi walifanya vizuri katika nafasi zao bila degree. Akiwa wizara ya mambo ya ndani, Mrema alifanya kazi nzuri na hakuna aliyevunja rekodi yake mpaka sasa. Hakuwa na shahada wala kishada. Mzee Mwinyi aliongoza nchi kwa busara na hekima kubwa bila kuwa na 'degree wala nini.

Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.

Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters?!

Tujiulize wabunge au mawaziri wenye degrees wamefanya nini cha maana. Wame add value gani? Au wamezikimbia tu taaluma zao kifuata maslahi bungeni?

Mamlaka ziwe makini zinapompima mtu based on elimu pekee. Waende beyond vyeti. Kwa mfano haikuwa busara kuwatoa madereva wazoefu kazini eti kwa vile tu hawakuwa na chetu cha form 4.

Sioni mantiki ya kumwamini zaidi dereva mpya kwa vile tu amemaliza kipato cha nne ukamwacha mzoefu wa miaka 20!

Hii homa homa ya shahada na PhDs inahitaji vidonge. Shahada haikufanyi kuwa nesi mzuri zaidi kama huna wito na kazi hiyo.

Wala uprofesa haukufanyi kuwa waziri bora zaidi kuliko akina Mzee Kawawa kama sio mzalendo. Vyeti havifanyi kazi. Get out of the bottle!!!
 
Kama ana PhD ya kweli na awe na kipaji cha siasa utafurahi. Mf waziri wa elimu akienda kuhutubia chuo kikuu anaona wote kama watoto tu "no inferiority complex "
 
Kwamba Msukuma Bungeni anaongea vya maana kulika Prof. Muhongo sio?

Sawa Bwana. Lakini unasindwa kutofautisha "kuongea sana" na kikicho ndani ya maongezi ya mtu!
 


Fahari ya mtanzania ni status kwa kujitengenezea PhD hata kama ni fake pamoja na vitambi bila kijali anacho deliver,
 
Hakuna watu kwenye beurocracy ndani ya serikali kama hawa wanaoitwa PhD holder. Unakuta mtu ni PhD holder halafu ni mkurugenzi wa H/shauri. Anasubiria kupewa maagizo na form four failure ambaye ni mkuu wa wilaya.
 
Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters?

Msukuma ni mpiga kelele mzuri lakini sasa maji yamezidi unga; amekwenda kukopa kwenye mabenki na kufanya biashara bila kitabu na sasa mabenki yanakamata mali zake kwani kashindwa kurejesha mikopo!! Elimu ya darasa la saba hiyo.
 
bado hujaongea hoja ya msingi, ni kama ulikuwa na point ila imeshindwa kabisa kiiwasilisha, na nahisi tatizo ni elimu, kama unasoma au unanafasi ya kusoma basi soma sana upate hiyo PhD, moja ya vitu vizuri dunia hii ya sasa ni kuwa na elimu
 
Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.
Huo utafiti umeufanya lini?
 
Inferiority complex inamsumbua mleta uzi, go back to school mkuu... Wakati tukiambiwa nenda shule wengine wakakimbia umande then now wanakula mema ya nchi kwa mwamvuli wa PhD zao you have to keep quiet and struggle...
 
Kama ana PhD ya kweli na awe na kipaji cha siasa utafurahi. Mf waziri wa elimu akienda kuhutubia chuo kikuu anaona wote kama watoto tu "no inferiority complex "
Kasomea shahada zote zinazofundishwa chuo kikuu hata awe na dharau? Ana PhD katika nyanja moja tu, iweje ajione yeye ndio awaye yote?
 
Hizi
PhD zilisomwa Kwa lugha gani!?? Mbona kukizunguza ni mtihani!??
Ndio hapo sasa! PhD sio ya kulikomboa taifa na jamii kwa huo ujuzi wake, bali ni sifa tu kuwa naye ana PhD!
 
Inferiority complex inamsumbua mleta uzi, go back to school mkuu... Wakati tukiambiwa nenda shule wengine wakakimbia umande then now wanakula mema ya nchi kwa mwamvuli wa PhD zao you have to keep quiet and struggle...

Nimesoma vya kutosha clown. Niende mara ngapiii....
 
Serikali ikiacha wasomi mnaanza tena kusema serikali imedharau wasomi inachagua failures...

Unafki ni mmbaya sana.
 
Nimesoma vya kutosha clown. Niende mara ngapiii....
Then stop dissing... Sio kila mwenye PhD hana knowledge au karama ya uongozi na sio kila asiye na PhD ana karama au knowledge ya uongozi... Kila zama na watu wake, enzi za Nyerere ni waaaaay different than enzi hizi za JPM, learn to differentiate eras
 
Jamaa kajaza ma.PhD holders kwenye utawala wake akidhani ndio suluhisho. Sidhani kama Prof. Ndalichako is being a better education minister than Mama Sitta eti kwa sababu ni pro. Ubabaishaji mtupu
 

Advice noted. I appreciate
 
Jamaa kajaza ma.PhD holders kwenye utawala wake akidhani ndio suluhisho. Sidhani kama Prof. Ndalichako is being a better education minister than Mama Sitta eti kwa sababu ni pro. Ubabaishaji mtupu
"Profesa" wa sifuri?!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…