Dhana halisi ya mlango, kila mtu aweze pita,
Asikunje hata mgongo, ndani aweze kukita,
Alisema manifongo, ingia usijejuta,
Kuweka kitasa ni ubinafsi, acha mlango wazi majirani tuingie.
Wewe pia meingia, wengi umewakamua,
Mlango haukuzuia, ndani ulipekenyua,
Juuu wapumulia, leo walia ka mvua,
Boko ala wenziwe, lakini nae aliwa
Kama wewe umepita, acha na sisi tuonje,
Kwa hiari sio vita, ingia na utoke nje,
Using'ang'anie kuta, ubabe kama Sizonje,
Ingia ndani, maliza halafu toka nje na wenzio waweze kuingia