Sina hakika kama hili limeshapatiwa ufumbuzi lakini kuna kero nyengine pale darajani kwa nyakati za usiku. Taa karibu zote zimeshaungua kuna baadhi tu ndio zinawaka. Sasa naona mamlaka zinazohusika zingeweka taa za solar na kuondoa hizi za kawaida kwani japo nyingi zimeshakufa lakini kwakuwa zinategemea umeme huu wa kawaida pindi unaponatika panakuwa sehemu hatarishi tofauti na pale mwanzo wakati taa zote zinawaka palikuwana mvuto mzuri sana nyakati za usiku.
Naomba kuwasilisha kwa taarifa na hatua.
Sent from my iPhone using JamiiForums