Usaili wa Kada ya Pharmaceutical Technician 2

Abdul kalaam

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2017
Posts
446
Reaction score
568
Habari,

Mimi ni kijana ambae nimechaguliwa kufanya usaili kada ya pharmaceutical technician hospitali fulani.

Ombi langu kwenu kwa ambao tayari muna uzoefu wa hizi saili naomba munielekeze yafuatayo.

1. Jinsi ya kujibu maswali ya written, tunajaza kwa mfumo wa essay au numbering/mention?

2. Naomba kujua maswali common ambayo wanapendelea kuuliza kwenye (topics ambazo wanapenda kutoa maswali).

3. Aina ya maswali ambayo wanauliza kwenye oral interview.

4. Vitu gani vya kuzingatia ili niweze kufaulu.

Asanten sana.
natumaini nitapata maelezo ambayo yanaweza nisaidie mimi na wengine kubadili maisha yao kupitia ajira za utumishi.
 
Soma x ray tube ,part zake na ujue kuielezea vzuri ...

Jua vifaaa mbali mbali vya maabara vinavyosaidia kutibu watu wenye cancer ,mvunjiko wa ndani kwa ndani ,..

Hizo ni possible tu [emoji23]
 
Jikumbushe mambo yote katika kada yako huku ukibase kwenye knowledge ya utendaji kazi.

Kama unajua kuandika haraka na points zinatiririka kama maji, unaweza kuandika essay ndani ya dk 10 kwa swali.

Kama huwezi hilo andika point kwa ufupi. Muda huwa ni kidogo
 
soma sana kama vile unaenda kupiga paper ulivyokuwa chuoni unasoma
 
VP kuhusu institutions ambayo ndio muajiri labda mfano PURA, kuna haja ya kuisoma na yenyewe hasa kwenye writen?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
taasisi kama taasisi sio lazima labda uisome kwa interest za kuijua zaidi sana sana soma majukumu ya kazi uiyoiomba kwenye hiyo taasisi , maswali mengi kwenye interview ni professiona zaidi ni vitu uivyojifunza darasani
 
Kwahyo unaweza kueleza kwa kuweka Roman kwa point na maelezo kidogo au sio mkuu..?
 
1a. Muombe Mungu sana.
1b. Soma mambo common ya kada yako. Pia soma na basic concepts za research.

2. Andika point na uelezee kidogo na ukiweza toa na mfano.

3. Mkono uchangamke kama typewriter kweli kweli. Dk 40 sio nyingi ukizichukulia poa!

4. Kuhusu taasisi soma labda kwa ajili ya oral na sio written.

5. Kamwe usiache kujibu swali lolote. Jibu maswali yote vile unavoelewa.
 
Nakazia hapo namba 5. Usiache swali jibu maswali yote ,ukiacha imekula kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…