Moja ya vitu vinachonishangaza sana kuhusu USA, ni kuhusu Miji yao, unasikia Mji una jina kubwa na kujulikana Dunia nzima lkn ukiangalia una watu wachache tu, kwa mfano San Fransisco pmj na umaarufu wake lkn una watu laki 8 tu, New York City una watu chini ya milioni 9 kumbuka USA ina wakazi zaidi ya milioni 300, wkt TZ yetu Dar peke yake ina watu zaidi ya Milioni 5, idadi kamili hakuna mtu anajua!
Hivyo nafikiri ingekuwa vyema tukaiga hilo, tufungue economic centers nchi nzima, kwa mfano Mbeya iwe economic center ya huko Kusini Magharibi, labda Tabora/KGM iwe kati, Mtwara iwe Kusini Mashariki, Mwanza iwe Kaskazini n.k. na huko kote kuwe kama Dar hapo tutaweza kuwa kama USA 🙂