USA intervention

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
909
MAREKANI NI TAIFA BABE,VAMIZI NA HARAMIA, MASLAHI YAKE POPOTE DUNIANI IMEKUWA CHANZO CHA MIGOGORO ULIMWENGUNI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Friday -22/3/2019.
Dumila -Kilosa,Morogoro-Tanzania.

Marekani ndio taifa kiranja duniani, utekelezaji wa mamlaka yake katika kuisimamia dunia katika Nyanja za kiusalama na kijasusi, kupitia ujasusi umeifanya dunia kuwa sio sehemu salama kabisa, upenyezaji wa maslahi ya taifa hilo kwa kutekeleza dhana ya kupandikiza viongozi kwa kulinda maslahi ya taifa hilo umeongeza umwagikaji wa damu za binadamu duniani, takwimu huonesha kwamba toka 1945 mpaka sasa zaidi ya watu milioni 200 wamepoteza maisha kwa sababu zitokanazo na mkono wa taifa hilo.

Katika msingi huu umeifanya Marekani kuendelea kuwa taifa hatari kwa mustakabari wa amani ya dunia, Hata hivyo hiyo aijawa tatizo kwa Marekani kwani bado mpaka sasa imeendelea kuhakikisha maslahi yake yanakuwa ndio kipaubele kwake, jambo ambalo imeifanya kuendelea kutekeleza njia za kiharamia popote duniani kwa kupitia kisingizio cha demokrasia au mapinduzi.

Kupitia makala hii leo tutaona ni namna gani Marekani inavyo tekeleza uharamia wake kwa kulinda maslahi yake wakati wa kutaka kutekeleza njia za kupachika vibaraka watakao rudisha fadhila na kusimamia masrahi ya Marekani, taifa hili hutumia njia za kijasusi kubalance masrahi yake duniani. Nataka nikuoneshe mission zilizofanywa na Marekani kupitia CIA baada ya Vita Kuu ya II ya dunia kwa lengo la kupachika viongozi kanzu. Hatua hizi kawaida hutumia mfumo wa mapinduzi ya kuziondoa serikali halali zilizochaguliwa kidemokrasia na kisha kuunda serikali za mrengo wa wao ambazo zitalinda maslahi ya biashara ya Marekani.

Mara nyingi, kwa kushangaza, serikali ya mrengo wa kulia wanazoziweka hufanya ukiukwaji wa haki za binadamu na kuishia kuwa tishio kubwa kwa maslahi ya biashara ya Marekani baadae na kisha baadae huwaondoa au kuwataka watekeleze makubaliano yenye manufaa na Marekani ikiwa itaonekana kushindwa kutekeleza masrahi ya Marekani basi husababishiwa vita na Marekani na mwisho utawala huo uondolewa.

Nilichagua kueleza makala hii kipindi hichi ambacho tumeona sarakasi nyingi huko Venezuela dhidi ya Marekani, kwakuwa pia nimeona mataifa ya Afrika sasa yanajipenyeza kwa mbia mwingine mpya ambaye ni Mchina kwa kasi sana jambo lilo zidisha vita ya kibiashara baina ya Marekani na Uchina, hivyo andiko hili litaangazia Marekani kwakuwa kipindi cha baada ya WWII hali ya hewa ya kibeberu ilianza kubadilika, kwa kuvutana juu ya ustawi wa kikomunisti au demokrasia ya kweli kwa wakati huo.

Ukoministi wakati huo ulionekana kama tishio zaidi duniani hasa kwa maslahi ya Marekani jambo lilomfanya Marekani aongeze juhudi ya kupambana bila kujali utu ili mradi masrahi yake yana fika salama Washington

Wakati wa kuiandaa makala hii nimefanya utafiti katika vyanzo mbalimbali moja ya Vyanzo vilio niongoza karibu 30% kukamilasha makala hii ni pamoja na kutoka kwenye jarida la “Killing Hope”: Majeshi ya Marekani na C.I.A. Hatua tangu Vita Kuu ya II ya dunia pamoja na website ya http://www.us-uk-interventions.org

Kupitia tishio la Usoviet na hofu ya kupoteza turufu ya Marekani pamoja na maslahi yake Marekani iletekeleza mapinduzi ama kuwauwa viongozi walio onekani hatarishi katika masrahi yake au kuvuruga nchi hizo zisitawalike ili iwe rahisi kupenyeza turufu ya masrahi yake. Zifuatazo ni nchi amabzo Marekani iliingilia (intervention) ili kuhakikisha masrahi yake hayapotei.

CHINA: Kati ya mwaka wa 1945 na 1949, Marekani iliingilia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huko China kwa kukipa sapoti chama cha Kumitong dhidi ya chama cha Kikoministi, Marekani iliamua kuchukua upande wa Chiang Kai-shek dhidi ya wanakomunisti, ingawa wanakomunisti walikuwa karibu sana wa Marekani kabla ya Mao ze dong kuanza kuegemea kwenye siasa za Usoviet.

UGIRIKI: Kati ya 1944 na 1947, Georgios Papandreou anakuwa waziri mkuu wa Ugiriki kwa kushinda kura nyingi chini ya usimamizi wa Uingereza. Wahamiaji nchini walianza kupinga hii kwa Uingereza kuingilia uchaguzi huo. Baadae Usovieti ikaingilia katika uchaguzi huo na kuunga mkono vyama vya Royalist. Marekani ilipoona hilo iliamua kuunga mkono nguvu za mrengo wa kulia ili kuwashinda siasa za mlengo wa mkono wa shoto.

Vita vya kisiasa vikazuka na mivutano ya kutishia kuchafua nchi ya Kigiriki vikaibuka kati ya vikosi vya mrengo wa Marekani na Uingereza vinavyoungwa mkono na Umoja wa Kidemokrasia ya Ugiriki kwa upande mmoja, na ule ulioungwa mkono na Yugoslavia, Albania na Bulgaria chini ya msukumo wa Usoviet, kufatia hatua hii ikazuka vita vya kwanza vya kisiasa Ugiriki chini ya mwamvuli wa vita Baridi (Cold War). Hata hivyo baadae Georgios Papandreou alishinda kwa usimamizi wa Marekani japo Mwaka wa 1965, CIA ilisaidia tena kumuondoa Georgios Papandreou kwa kushindwa kuunga mkono maslahi ya Marekani pale alipogeuka na kuunga siasa za Usoviet.

PHILIPINES: Mapema miaka ya 1900, Marekani ilipata udhibiti wa Ufilipino baada ya vita vya Hispania na Marekani kumalizika na kupelekea kuuawa kwa watu wapatao 600,000 raia wa Filipino. Mnamo mwaka wa 1941, Japan nayo ikashindwa vita na kukimbia Philippines. Kuanzia 1945 hadi 1953, jeshi la Marekani liliendelea kujitanua nchini Philipino huku ikiendelea kupigana dhidi ya vikosi vya mgambo vya leftist (Huks) kikundi hichi cha Huks kilikuwa kikitetea udhibiti wa nchi hiyo toka kipindi cha wavamizi wa Kijapani. Baada ya vita kati ya Marekani kupigana na askali wa ukombozi wa Wahuki, Marekani ilishinda vita hivyo na kisha wakapandikiza kiongozi wao wa kidikteta aliyeitwa Ferdinand Marcos aliyesimamia maslahi yao.

KOREA KUSINI: Baada ya Japan kujitoa udhibiti wake juu ya Korea mwaka 1945, serikali ya muda ilianzishwa kabla ya kupata uhuru kamili. Ingawa makubaliano yalifanywa kuwa Umoja wa Sovieti utaondoka Korea ya Kaskazini na Marekani zitatoka Korea ya Kusini, Marekani ilishindwa kutekeleza hilo na ilianza kupandikiza serekali ya kijeshi wenye siasa za mrengo wa kulia nchini Korea kusini ambao Marekani walishirikiana na serikali ya Kijapani kuidhibiti Korea kusini toka hapo utawala wa Korea kusini umekuwa ukifuata maagizo ya Washington.

ALBANIA: Kuanzia 1949 hadi 1953, Marekani na Uingereza walifanya majaribio yaliyofanikiwa ya kupindua serikali ya kikomunisti na kuanzisha serikali ya washirika wao ya kifalme iliyo dumu kwa miongo kadhaa kwa msrahi yao.

ITALIA: Mwaka wa 1948, CIA inadukua uchaguzi wa kidemokrasia ili kuzuia Chama cha Kikomunisti kuchukua mamlaka. Marekani ilimpadikiza Gladio aweze kusalia madalakani kwa kutumia kisingizio cha hali ya hatari, CIA ilihusika kuweza kuifanya serikali pandikizi ya Gradio kubakia madarakani katika Italia wakidai kuwa kuna uwezekano wa uvamizi kutoka Urusi.

IRAN: Mnamo mwaka wa 1953 serikali ya Mossadegh ilishambuliwa baada ya kutishia kusimamisha makampuni ya mafuta ya Uingereza. CIA ikasuka mipango na kufanikisha kumuingiza madarakani Shah, kuanzia hapo, kipindi chote cha utawala wa Shah cha miaka 25 Irani imeshuhudia ukiukwaji wa haki za binadamu na mateso huko Iran, ila Marekani ilibakia kimya kwakuwa ilikuwa ikifaidika na mafuta ya taifa hilo kwakua Marekani ilishikilia umiliki wa asilimia 40 ya sekta yao ya mafuta. Baada ya mapinduzi ya 1979 ambayo yalisababisha kuundwa kwa Jamuhuri ya kislamu chini ya Ayatollah Khumen bado Marekani imeendelea kujaribu udhibiti wa Iran mpaka sasa.

GUATEMALA: Mnamo mwaka wa 1954, Marekani kupitia CIA ilimfukuza madarakani Jacob Arbenz aliyechaguliwa kidemokrasi kwa sababu alishindwa kuimarisha Kampuni ya Umoja wa Matunda iliyokuwa nchini Guetamala chini ya umiliki wa Wamarekani, ambapo mkurugenzi wa CIA Allen Dulles alikuwa na hisa. Kufatia hiyo Marekani ilipandikiza Serikali ya mrengo wake ambayo ilitawala kwa karibu miaka 30, serikali hiyo ilifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa jamii ya Meya na Marekani iliijua hilo lakini iliunga mkono.

VIETINAM KUSINI: Mwaka wa 1949, Marekani inaamua kutoa msaada kwa Ufaransa katika vita vya Vietnam. Ufaransa ilipigana vita ile kuzuia upanuzi wa Kikomunisti badala ya vita vya kikoloni kumalizika. Ingawa Wafaransa walishindwa vita ile na kutakiwa kufikia makubaliano ya amani ya Geneva, Lakini Ngo Dinh Diem anakataa kuheshimu makubaliano na kuomba msaada wa Marekani kusaidia (1954-1958). Utawala wa Diem na Marekani wanaingia vitani kukabiliana na Vietinam Kusini juu ya Vietnam Kaskazini. Hii inapelekea kuibuka kwa vita vya Vietnam. Mnamo mwaka wa 1967 Marekani inawasaidia wanamgambo wa Vietnam Kaskazini kuwakabili wanamgambo wa Viet Cong, na kusababisha mauaji ya karibu watu 20,000 japo kuwa mwisho wa vita hivi Marekani ilishindwa vita hivi na kuondoa majeshi yake.

LAOS: Kati ya 1957 na 1963, CIA inajaribu kuunda makundi kadhaa ya kuvuruga uchaguzi wa kidemokrasia, iliposhindwa ikaamua kujenga jeshi la siri ili kushambulia serikali ya mlengo wa kushoto ya Pathet Lao iliyo ungwa mkono na Usoviet. Baada ya jeshi la Marekani kushindwa Kuvamia, Marekani wanaamua kutoa Mabomu ya ardhini kalibu tani milioni 2 za mabomu kwa vikosi vya wasi. Kufatia mabomu hayo kusambazwa ilipelekea Laos kuwa na kumbukumbu ya kua nchi yenye idadi kubwa zaidi ya mabomu yaliyotegwa ardhini duniani.

Haiti: Mwaka wa 1959, Marekani inasaidia kumuingiza madarakani dictator Duvalier, ambaye anaua zaidi ya watu 100,000 na mapanga (machete) kupitia operation yake akiwatumia polisi. Kufatia mauaji hayo, Mwaka wa 1986, uasi mkubwa dhidi ya Duvalier ukaibuka, baada ya kuonekana hali hiyo Marekani ikaamua kumuhamisha Ufaransa kwa kisingizio cha kustaafu. Na Marekani inaamua tena kusimamia uchaguzi wa dikteta mwingine wa mrengo wa kulia mnamo 1990, baada ya mgombea wa mlengo wa kushoto kushinda kwa asilimia 68 ya kura, Marekani inamua kiingia kijeshi kupitia ujasusi ulio sukwa na CIA .

Cuba: Mnamo mwaka wa 1961, CIA inajaribu kuivamia Cuba kwa kuwatumia wakimbizi wa kicuba ambao walikuwa mafia, wateswaji, wamiliki wa biashara matajiri, na maofisa wa kijeshi kutoka serikali ya Batista, ili kusababisha uasi dhidi ya Castro. Jaribio hili halikufanikiwa japo Marekani ilikuwa ikijaribu kutekeleza uharamia cuba kila mara toka mwaka 1961 mpaka mwaka 1999.

Jamhuri ya Dominikani: Mwaka wa 1961, CIA walitekereza operation ya kumuua Rafael Trujillo, ambaye utawala wake ulikuwa wa kikatili, mwanzoni walimsaidia kwa miaka mingi lakini baadae alianza kushindana na maslahi ya Marekani. Mnamo mwaka wa 1963, walimuunga mkono Juan Bosch wa mrengo wa kidemokrasia na kuanzisha utawala wa mrengo wa kulia. CIA ilizima jaribio la uasi la mwaka wa 1965 lilompindua Boch na kumrejesha tena madarakani Juan Bosch.

Ecuador: Mwaka wa 1961, CIA ilipelekea rais aliyechaguliwa kidemokrasia Jose Velasco kujiuzulu. Makamu wa Rais Carlose Arosemana akashika nchi na kuamua kuchagua kuwa upandae wa CIA, lakini Mnamo mwaka wa 1963, anapinduliwa kijeshi na kikosi cha uasi kutoka jeshi la Ecuador kilichoungwa mkono na Marekani baada ya kuishtaki serikali ya Marekani. Mapinduzi hayo ni yale ilikuwa sehemu ya “Operesheni Condor”, ambayo ilikuwa ni kampeni ya kupambana na serikali za kikomunisti katika nchi za Amerika Kusini ili kuzuia wapinzani wa kisiasa.

Congo: mwaka 1961, CIA waliratibu mapinduzi na mauaji ya waziri mkuu wa kwanza wa kongo Patrice Lumumba mkakati huo wa kukatisha maisha ya lumumba ulipewa jina operation Barracuda, na baadae mwaka 1965, Marekani ilimpachika Mobutu Sese Seko. Ambae alikuwa kibaraka na kiongozi aliye ongoza kwa rushwa,ukandamizaji na utawala mbovu.

Paraguay: Toka 1962 mpaka 1975, mtawala wa kifascist Afredo Stroessner alipokea 146 million kutoka Marekani, kama msaada wa kuendesha mapinduzi yaliyofanikiwa kuiondoa serikali halali madarakani. Katika utawala wake Marekani iliiuunga mkono, utawala huu uligubikwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, mauaji ya kimbali kwa raia wa asili ya Paraguay, nchi ikawa soko la madawa yakulevya na genge la wauza madawa kutoka Marekani, nchi ikawa kituo cha silaha kupitishwa kwenda kuuziwa waasi.

Brazil: mwaka 1964, CIA walifadhili utekelezaji wa mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya iliyochaguliwa kihalali kupitia mfumo wa demokrasia (democratically election) chini ya Joao Goulart na jeshi kuongoza nchi chini ya dikiteta General Castelo Branco ambae aliongoza nchi katika wakati unaotajwa kama zama za maangamizi nchini Brazil. Nchi ya Marekani iliisapoti utawala wake kwa kutegemea maslahi ya Washington. Hivyo utawala huu ulidhamilia kumaliza wafuasi wote wa mlengo wa communists nchini humo.

Indonesia: mwaka 1965, CIA walitekeleza mapinduzi dhidi ya serikali ya Sukarno. Mpango huu waliupanga na kuutekeleza toka 1957, mapinduzi hayo yalimuuingiza madarakani, General Suharto, ambae kwa msaada wa Marekani alitekeleza mauaji zaidi ya watu 500,000 huku watu zaidi ya 3 million waliwekwa kizuizini ama kufungwa kwa makosa ya kuwa wafuasi wa mlengo wa ukommunists. Na kwa kipindi chote hicho CIA ilisadia utawala wake kutekeleza mauuaji dhidi ya maadui wa Suhaartoi.

Ghana: mwaka 1966, Marekani ilisaidia kumuondosha madarakani mwanamajumui wa Afrika, Kwame Nkrumah na kuingiza serikali ya kibaraka wao chini ya General Kotoka.

Israel na Palestine: toka mwaka 1967 mpaka sasa, Marekani imekuwa ni mfadhiri mkubwa wa serikali ya Israel katika kuongeza ukaliaji wa eneo la Palestine. Marekani imekuwa ikifanya hivyo kwa kuongeza kiasi cha fedha katika kuhakikisha ukaliaji wa eneo la Palestine unadhibitiwa na Israel.

Bolivia: mwaka 1967, Che Guevera aliuwawa katika aridhi ya Bolivian na asikali wa kibolivia waliokuwa wakipata mafunzo kutoka kwa askali wa Marekani walioitwa US Green Berets kwa ushirikiano mkubwa na CIA. Pia mwaka 1971 katika taifa hilo hilo la Bolivia, CIA walitekeleza mapinduzi na kumuondoa madarakani raisi Juan Torres. Nakumuingiza madarakani dictator Hugo Banzer, katika utawala wake wapinzani wake karibu 2,000 walitupwa jera bila kupitia mahakamani, wengine waliteswa,huku wanawake wakibakwa hovyo, na wengi waliuwawa kwa kunyongwa. Na mwaka 1982, pia baada ya utawala wake kupoteza ushawishi na Washington CIA walishiriki kumuondoa na kumpachika Celso Torrelio.

Cambodia: mwaka 1970, CIA walishiliki katika njama ya kumpindua Prince Sahounek, ambae alichangia pakubwa katika kuimaliza vita ya Vietnam katika kupeleka msaada wa askali wa Cambodians kusaidia katika vita ya Vietnam War. Alipoondolewa, CIA wakampachika Lon Nol.

Chile: CIA walishiliki njama za kuiondoa serikali ya kidemokrasia na kutekeleza mauaji ya raisi Salvador Allende mwaka 1973, huyu Allende alipinga Marekani kuinyonya chile kupitia mpango wa kubinafsisha makampuni ya umma ya Chile, mapinduzi hayo yalimuingiza madarakani Augusto Pinochet, kiongozo muuaji,na mfujaji wa mali za umma aliyepitiliza.

Australia: mwaka 1975, CIA walishiriki katiaka kumuondoa madarakani waziri mkuu Edward Whitlam ambae alikuwa na siasa za mlengo wa kushoto. Kwa kushilikiana na Governor General John Kerr, ambae alikubali kutekeleza mpango uliosukwa na CIA kwa kutumia sheria ya (archaic law ) ambayo ilitumiwa kumuondoa Whitlam, hata hivyo ilikuwa makosa kuondolewa kwake kwakua waziri mkuu ni kiongozi anae chaguliwa kidemokrasia huku Governor General ni mteule wa Malikia (Is appointed by the Queen).

Angola: mwaka 1975, CIA walifadhiri vita nchini Angola kwa kupambana na communism. Hii ilipelekea wafuasi wa ukominist nao kufadhiri vita upande wao kwa kupewa nguvu na mataifa ya Cuba na Soviet Union. Vita hivi viliigharimu Angola kwani zaidi ya watu 300,000 walipoteza maisha.

Portugal: mwaka 1975, CIA walitekereza jaribio la mapinduzi lilounga mkono siasa za mlengo wa kulia liloongozwa na General Vasco dos Santos Goncalves.

Jamaica: toka mwaka 1976 mpaka 1980, CIA walijaribu bila mafanikio kufanya usaidizi wa kuipindua serikali ya Michael Manley. Katika uchaguzi wa 1980 akashindwa uchaguzi baada ya figisu za Marekani , lakin alilejea tena madarakani mwaka 1989 baada ya kukubali kufuata masharti ya Washington.

El Salvador: Ingawa serikali ya mrengo wa kulia ilipinduluwa mwaka wa 1979, Marekani iliendelea kuisaidia serikali ya kijeshi iliyo tii amri za washington. Mwaka 1980, Askofu Mkuu, wa El Salvador Oscar Romero, alitoa ombi kumtaka raisi wa Marekani Rais Carter kuacha kuisaidia serikali ya El Salvador kuua watu wake. Cha kushangaza Romero alipigwa risasi katikati ya Misa kanisani kwake na kiongozi wa taifa hilo wa mrengo wa kulia Roberto D'Aubuisson. Mauaji haya yalisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa. Marekani iliendelea kusambaza siraha na mafunzo kwa serikali ili kutekeleza mauaji. Vita iliisha mwaka 1992, huku zaidi ya watu 63,000 raia wa Salvador waliuawa.

Nicaragua: Mwaka wa 1979, dikteta aliyepachikwa na CIA Samoza aliangushwa kutokana na uasi mkubwa uliotokea, na Sandinistas mfuasi wa UMarxist kuchukua serikali. Lakini kufatia hali hiyo Maafisa wa jeshi la wakati wa utawala wa Samoza walijiunga na Contras ambae aliungwa mkono na CIA, ambaye alianzisha vita dhidi ya Sandinistas. CIA ilimtumia fedha iliyotokana na biashara ya kocaini iliyofanyika nchini humo Nicaragua, ili kutoa msaada wa kifedha kwa Contras. Mnamo mwaka 1986,serikali ya Nicaragua chini ya Sandinista iliitungua ndege ya CIA ya kubeba vifaa vya kijeshi kwa Contras, ikitoa ushahidi kwamba CIA ilikuwa imetoa silaha kwa Contras, Marekani ilikanusha na dunia haikusema chochote.

Chadi: Kuanzia mwaka 1982 hadi 1990, Marekani ilimuunga mkono Hissene Habre, na kumpigia debe katika uchaguzi nchini humo. Ikumbukwe kuwa huyu Habre alipatikana na hatia ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na ubakaji, utumwa wa kijinsia na mauaji ya watu 40,000 katika mahakama za kimataifa.

Honduras: Mwaka wa 1983, CIA ilisaidia kutoa vifaa vya kufundisha maafisa walioasi jeshi. Waasi ao walijulikana kama Bondlion waasi hawa waliuwa maerfu ya watu nchini Honduras.

Panama: Marekani imeweka askari wake huko Panama tangu mwanzo mwa miaka ya 1900, Mnamo 1984, Marekani ilisaidia kufanya udanganyifu wa uchaguzi ili kumpata mtu wao, ilimuingiza madarakani Manuel Noriega kinguvu. Lakini mnamo mwaka wa 1989, Marekani tena ilishiriki kumuodoa madarakani General Manuel Noriega baada ya kutofautina nae kufatia kudhibiti biashara ya mihadarati (MADAHA) nchini humo.

Venezuela: Mnamo mwaka 2002, Marekani imeshiriki katika kutekeleza mapinduzi ambayo yalilenga kumuondoa Hugo Chavez. Hata hivyo wafuasi wa Chavez walikuwa na nguvu sana hivyo ndani ya siku 3 mapinduzi yalizimwa na Chavez kureje madarakani. Tangu mwaka 2009, Marekani imetayarisha dola 49 milioni kwa upinzani wa Venezuela ili kumuondosha madarakani Maduro.

Mexiko: Serikali ya Marekani ilidhibiti uchaguzi wa mwaka 2006. Ingawa uchaguzi ulimpa ushindi Andres Manuel Lopez Obrador, lakini Felipe Calderon ndie aliyepewa ushindi huyu alikuwa mshirika wa Marekani. Na hii ilitokana kuwa Calderon alitumia fedha iliyo muingiza madarakani iliyofadhiliwa kutoka Marekani. Mnamo mwaka 2012, ripoti ilionyesha kuwa vita vya madawa ya kulevya vya Marekani vinahusika katika kuua watu zaidi ya 120,000 tangu Calderon alipo ianzisha na mshirika wake Marekani.

Mashariki ya Kati: vikundi vingi vya Marekani vimepachikwa na kupewa silaha na mafunzo kama vile al-Qaeda na ISIS. Hata huko Syria, kuna ushahidi unaonyesha kwamba Marekani imetoa fedha nyingi na kuviunga mkono vikundi kama vile al-Nusra Front.

Afghanistan: hapa CIA ilianza mnamo mwaka wa 1979 na mpango wa kufadhili wanamgambo wa Mujahideen ili kuidhibiti serikali ya Kikomunisti ya Kidemokrasia ya Afghanistan. katika kipindi hicho CIA iliwafundisha zaidi ya wapiganaji 100,000 kupigana na Soviet na serikali ya Kikomunisti ya Afghanistan ili kuusambaratisha USSR.

Grenada: Mwishoni mwa miaka ya 1984, uchaguzi uliofanyika kiongozi mfuasi wa Marekani alishinda na aliungwa mkono na utawala wa Reagan. Mwaka mmoja baadaye, shirika la haki za binadamu, Baraza la Masuala ya Ulimwengu, liliripoti kuwa Grenada imebadilika kuwa eneo la soko la silaha, mahali palipo kithiri kwa ukatili wa raia, kukamatwa kwa wananchi kiholela, matumizi mabaya ya mamlaka, na uharibifu mkubwa wa taifa kwa ufujaji wa mali za umma.

Hizi ni baadhi ya nchi ambazo Marekani ilifanya uingiliaji (intervention) ili kulinda maslahi yake, bila kujari madhara yatakayotokea. Toka hapo mapaka sasa kumekuwa na utumiaji wa mabavu wa Marekani katika kuiingilia mataifa mengi duniani, tumeliona hilo Iraq ,Libya, Syria, Iran na sasa Venezuela.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
 
Summarize habari yako. Mtu smart hawezi poteza muda kusoma.
 
Utajiri na ukafiri nyuma yake
 
Habari yako imejaa mahaba kwa Rusia .Hamna cha maana ulicho andika umepoteza mda bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…