Upinzani unakufa au CCM kinakufa?

Ninaamini Magufuli akikaza buti ccm itakufa.Kwa sababu hakuna aliye msafi. Hakuna ambaye ni salama mpaka sasa. Naikumbuka vita ya sokoine (RIP)na wahujumu uchumi,ilikuwa ni nchi nzima wahujumu waliwekwa ndani lakini.........

Sisi tunaamini Pombe anairudisha CCM ya Mwalimu.
 
CCM ni Magufuli na Magufuli ndo CCM kwasasa. Aliyeshinda uchaguzi ni Magufuli sio CCM. CCM halisi kwa sasa ni akina Lukuvi, Makamba Sn, Kinana, Nape, Mangula, Butiku, Mwigulu, Chenge, Karamagi, Diallo, na wazee Mwinyi, Mkapa na Kikwete ambao wameshindwa kuzikonga nyoto za watanzania hadi ikawabidi waanze kutafuta mabadiliko nje ya CCM. Magufuli leo hii ameshaanza kuiudhi CCM pia kutokana na kasi yake ya kupambana na walanguzi ambao wengi wao wana uhusiano mkubwa na wanaopenda CCM
 
Wanaolia baada ya kushindwa kumbe ndio walioshinda uchaguzi? Huku sasa ni kufikiria 'kimasaburi". Namkumbusha mleta uzi kuwa kukataa wabunge wasiwe kwenye bodi za mashirika ya umma kulianzishwa na rais wa awamu ya pili Mzee AH Mwinyi ila baadaye ikasahaulika sasa Magufuli kairudisha.

Mara ya kwanza walisema ccm imesimamisha wagombea wawili wa urais,yaani magufuli ccm A na lowassa ni ccm B,ila nimegunduwa kwamba kumbe magufuli alikuwa mgombea wa UKAWA aliyenadiwa na ccm,asanteni ccm kwa kumpa promo magu mkidhani ni mwenzenu
 
mtoa mada tumekuelewa,ungenyamaza wakati uongee,ona sasa umeyamsha magamba vitandani kwenye drip ya kutwa mara tatu
 
endeleeni kujifariji lakini mtabaki wapinzani milele msipojitathimini.


Inakufa ccm
 
Complex mind- upinzani ni ideology tu, upinzani si majina ya vyama, upinzani utakuwepo miaka yote lakini vyama vitafutika vitazaliwa vyama vipya

mfano: Taa-tanu 1954-ccm i977- next??????

Kwa mazingira ya siasa za tanzania kuna mabadiliko yanakuja lazima yaje, kwa sasa kinachoangaliwa zaidi ni chama gani kimeshika dola
ccm wameshika dola, lakini matarajio yao sivyo walivyotegemea, muda mfupi ujao watakuwa wapinzani wa dola, na upinzani utakuwa pamoja na dola.

Kama siasa zinaongozwa na itikadi na sera hakuna upande utakufa milele si ccm wala upinzani, kama ccm ni wajamaa labda cdm ni mabepari-wajamaa sioni atkayekufa hapo


kwahiyo kama ushindani wa vyama ni wa kiitikadi na kisera hakuna atayekufa wote wataishi milele ila kwa majina ya vyama tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…