Ninahuzunishwa sana na jinsi ambavyo waalimu wa Tz wasivyojitambua. Waalimu wamesambaa nchi nzima na wamesambaa katika jamii kubwa isiyo na uelewa mkubwa wa yanayoendelea nchini. Waalimu wangekuwa aggressive vya kutosha wana uwezo wa kuamua nani atawale nchi hii. Viongozi wetu wanajua hilo, ndo maana hawawapi mwanya wa kuji-mobilise kiasi hicho. Wamewekewa waalimu wenzao Wilayani kwa ajili ya kuwakandamiza, kwani mnyanyasaji wa mwalimu ni mwalimu mwenzake. Wameanzisha CWT na kuwaweka mamluki wao kuakikisha waalimu hawafurukuti, moja ya mbinu ni kuhakikisha viongozi wao hawawi waalimu wenye taaluma ya juu, wakienda kupiga kura kwenye chama chao wanamchagua mwalimu wa primary kwa kuwa wao ndo wenye uwakilishi mkubwa. Ushauri wangu ni huu ni lazima kila mwalimu mmoja mmoja kujitambua binafsi na kuanza kupinga uonevu na unyanyasaji anaofanyiwa. Wewe uliyeleta hoja hii umechukua initiative gani binafsi kujikwamua na unyanyasaji huo?Pili, CWT inapaswa kufanyiwa revolution ili kuwa ni mikakati mipana na kutetea sio waalimu tu bali wananchi kwa ujumla, kama tutakumbuka vizuri vyama vya wafanyakazi vilikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru ktk nchi nyingi za Kiafrika, kwa nini sio CWT? Waondokane na tofauti walizonazo kulingana na elimu au ngazi ya elimu wanyofanyia kazi, kwani zipo tofauti kati ya waalimu wa Primary, sec, vyuo na wale wanaofanya kazi za uongozi.Tatu, CWT wanapaswa kuwaelimisha waalimu kujielewa, wajenge umoja katikati ya wanachama wote, wawe tayari kuwatetea wanachama wao kwa hali na mali. Haya malalamiko unayoleta hapa CWT wanayajua? Wamechukua hatua gani? Kumbuka waalimu karibu wote ni wanachama wa CWT na wanachangia chama hiki kwa fedha nyingi kila mwezi.TAFAKARI NA CHUKUA HATUA sio kulalamika.