KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 541
Nawapa 20000/= halafu nahama nyumba. Hawa jamaa wakiishiwa ni lazima watarudi tena kwa gea hiyo hiyo.... au watawatuma wengine.........Umehamia katika nyumba ambayo LUKU ya umeme imechezewa. Pia katika nyumba hiyo kuna wapangaji wengine wawili ambao mnatumia kwa pajomaja hiyo Luku. Na kwa utaratibu waliouweka ukakuta kuwa wanachangishana sh. 10,000 kwa kila mpangaji ili kununua umeme. Na umeme ukinunuliwa unaishia tar. 17 ya mwezi na kwa siku zilizo baki LUKU inasoma 00.00 kuonyesha kuwa umeme umekwisha lakini kwa vile imechezewa inaendelea tu kupitisha umeme.
Kutokana na matumizi yenu makubwa ya umeme unajikuta kuwa unafaidika sana na hako kautaratibu kwa vile unachangia hela kidogo kwenye matumizi ya umeme. Baada ya kuishi kwa miezi nane TANESCO wanakuja kuwakamata. Kwa vile wewe sio mmiliki wa ile nyumba unamtaarifu Mwenye nyumba ambaye nae anakuachia mzigo kuwa umalizane na Tanesco maana yeye hana taarifa kuwa LUKU yake imechezewa. Unakwenda kwa vijana wa TANESCO wanakwambia tuongee la sivyo suala liende ofisini ambako wana kutishia kuwa faini ni sh. 5,000,000. Na kigezo wanachotumia kukubana ni kuwa wewe unataarifa kuwa LUKU imechezewa au ni Mbovu na hujatoa taarifa Tanesco. Wana sajest uwapatie sh. 20,000 ili wakurudishie umeme na kwa sharti kwamba umtafute fundi aliyeichezea LUKU airudishe kwenye hali yake ya kawaida.
je utoe sh. 20,000 na urudishiwe umeme au suala lako lipelekwe TANESCo kwa maamuzi mengine?
Hakuna utata katika hilo. Ulishiriki wizi na unapaswa kuubeba mzigo ipaswavyo. Hii tabia chafu wabongo kupenda wizi wizi mimi siipendi. Unatarajia TANESCO wapate wapi hela wakati wewe unaiba umeme. Uliona LUKU inasoma zero lakini umeme upo, wala hushangai! Unatumia tu, halafu ati hauhusiki. wacha! sema vishoka wa TANESCO nao mafisadi tu, ingelikuwa mimi nawapeleka ofisini, faini 5 milioni. Ndio ujue wizi ndio unaoturudisha nyumba hapa bongo
Kumbuka ukihama unakwenda kwenye nyumba ambayo kwa matumizi yako utalazimika kulipia umeme kwa sh. 150,000 kwa mwezi maana Tanesco wame inflate bei ya umeme kutokana na gharama kubwa za uendeshaji zinazotokana na ufisadi wa IPTL, SONGAS etc.Nawapa 20000/= halafu nahama nyumba. Hawa jamaa wakiishiwa ni lazima watarudi tena kwa gea hiyo hiyo.... au watawatuma wengine.........