Kuna wachezaji wafuatao ambao katika timu zao walikuwa wakichezea nafasi za kiungo wa ulinzi namba 6 au kiungo ushambuliaji namba 8. Kwa maoni yangu mpaka wakati huu bado sijaona aina ya wachezaji wa kuwalinganisha nao. I wish hawa wachezaji wa soka wa nyakati hizi wangepata nafasi ya kuwaona nina imani wangejifunza vitu fulani adimu toka kwao.
1. Nicodemus Njohole - Simba
2. Ramadhani Lenny - Simba
3. Juma Mkambi - Yanga
4. Charles Boniface Mkwasa - Yanga
5. George Kulagwa - Simba
6. Athumani China - Yanga & Simba
7. Octavian Mrope - Majimaji
8. Hamis Thobias Gaga - Pilsner, Simba
9. Khalid Bitebo Zembwela - Pamba
10. Hussein Ngulungu - Pan African
11. Mohamed Yahya Tostao - Yanga & Pan African
12. Ezekiel Grayson " Jujuman" - Simba & Yanga
13. Issa Athuman Mgaya - RTC Kagera & Yanga
14. Ally Maumba - Coastal Union
15. Saidi George - Coastal Union
16. Charles Mngodo - CDA Dodoma
17. Aston Padon - Tukuyu Stars & Simba
18. Justin Mtekere - Tukuyu Stars & Yanga
Sasa mbona wengine ni mawinga? eg Justin Mtekere - Tukuyu Stars & Yanga, George Kulagwa - Simba Lakini una kumbukumbu nzuri mdau, tatizo siku hizi viongozi wote njaa kali wanaganga njaa. Enzi hizo Yanga yuko babu Viran hana njaa
Hussein Ngulunu na Ezekiel Greyson(RIP) walikuwa mawinga. Mohamed Tostao alikuwa mshambualiaji no. 9
Ngoja nikupe namba sita za enzi hizo Gilbert Mahinya - 6 Tulikuwa tunamwita " Machine" wa Yanga Abdulrahman Juma- 8 ya Yanga- Bingwa wa kupiga corner Khalid Abeid - 6 ya Simba ya uhakika Omar Gumbo - 6 Sunderland kabla haijaitwa Simba Mwabuda Muhaji - 6 ya African Sports Tanga