Habari za Asubuhi wadau Tumshukuru Muumba tumeamka salama,Tukiwa kwenye mapumziko na wengine tukijiandaa kwenda ibadani na wale tuliofunga Nimeona weekend yangu leo Nianze kwa Huyu Mnyama Adimu Duniani ambae wengi Hatumfahamu nadhani hapa kwetu hawapo. Ahsanteni Asbh njema….
.
Panda ni wanyama wanapatikana kwa wingi kusini mwa China.
Unaweza kuwatambua kwa madoa yao yenye rangi nyekundu na nyeusi yaliyozunguka mwili wao.
Panda anafika urefu mpaka mita1.9 na kg 110 mpaka115 kwa wanaume inaweza fika mpaka 160.
Wanafanana na paka kwa mwonekano wao ila wana tabia kama za nyani na ngedere.
Kuna aina mbili za Panda( weupe na weusi, na wekundu) ,hutofautishwa na majina Tu: Red Panda and Giant Panda,walio wengi ni Black and white.
Wapo kwenye kundi la Carnivora ila 99% ya chakula wanachokula ni Bamboo pia hawana simile na hii misosoi kama majani,nyama pia ukiwapa mayai,samaki magimbi,machungwa ndizi wanapokea na kula.
Panda anabalehe akifikisha umri kati ya miaka 4 mpaka 8. Kipindi cha March na May ndio kipindi ambacho Panda huwa wanafanya mchezo mbaya kwa muda wa siku 3 mpaka 4,Hiii hutokea mara moja kwa mwaka.
Wanafanyaje tendo la ndoa?
Hawana tofauti sana na Paka,wa kike huwa anatambaa chini taratibu huku akijiweka tayari tayari mara nyingi kichwa huwa wanainamisha chini kama Kuku Hapo kidume akiona kichwa chini anawahi kudandia kwa nyuma huku akiwa amemkumbatia jike( hii ni muhimu sana kwa fertilization).
Panda sio wa mchezo mchezo,Tendo lando ni kuanzia sekunde 30 mpaka dk.5 ndio ndio anaridhika! Na anaweza kuendelea hata Zaidi ya hapo akihisi fertilization bado.
Maajabu ya kuzaliana!
Panda huwa anazaa mapacha lakini cha kusikitisha mmoja lazima afe anabaki mmoja,unajua kwa nini?
Panda hana uwezo wa kuhifadhi chakula kama wanyama wengine,hivyo ana uwezo wa kulisha panda mmoja Tu na hata baba Panda yeye hana uwezo wa kutafuta chakula kwa ajili ya Panda hivyo basi kinachofanyika Mama Panda anaangalia kati ya wale panda aliozaa yupi Strong ndio anaaza kunyonyesha! Yule weak huwa anajifia Tu.
Panda anazaliwa na rangi ya pink,kipofu na pia anakuwa kibogoyo akiwa na kilo kuanzia 90 mpaka 130.
Panda wanapenda sana kucheza na watu lakini pia wana aibu sana anapendelea kuwa peke yake peke
yake Tu.
>Unajua kama Panda huwa anacheka kama Binadaamu? Asubuhi njema.....
.