Je? Unakumbuka zile kero!,ni kero ambazo ulikuwa unapokea sms kila mara kama umekula?,unafanya nini?
Zile kero ambazo unapigiwa simu kwa muda mrefu anataka aongee na wewe!,mara video call!,mara anakuja ghetto mara kwa mara!
Unakumbuka zile kero za wivu wa kijinga za mara kwa mara?
Unachoka na kero unamwache aende zake!sasa unajisikia huru sana unaona ni kama vile mzigo umeutua!
Kwa vile muda ni Mwalimu mzuri una move on!unajipongeza. Huku sasa hakuna tena kero!haupokei tena sms hadi utume wewe! Haupigiwi tena simu hadi upige wewe,hata ukituma na yakutolea haujibiwi chochote hadi upige simu baby umepokea?
Hapo sasa unaanza kujiuliza hivi na date na mdoli usipougeuza unaukuta vile vile! Sasa hivi sms unazopokea ni zile za tuma kwa namba hii jina litatoka M5 tena!,sms za Polisi za ndugu wananchi!,sms za tatu mzuka,sms za betting n.k!
Hapo sasa ndio unakumbuka zile za mwanzo hazikuwa kero bali ilikuwa ni thamani ya muda mtu aliyoamua kuwekeza kwako!utatamani upokee tena sms ya goodnight badala ya low battery please charge!
Tulifunze kujua alama za nyakati.
N:B ,sijawahi kuandika uzi mrefu hivi [emoji28]