Mhn! Kwa Libya ilikuwa tofauti. Kwanza mabilioni ya dollars alizokuwa ameweka kwenye mabenki huko Ulaya na pia other kwenye gold. Wananchi wa Libya walikuwa safi sana kiuchumi. Social services zao kama za Ulaya tu na zaidi. Aliona shida kuachia wapinzani.
Pia assets nyingi zilikuwa chini yake familia nk. However yeye mwenyewe alikuwa akiishi kwenye tent.
Pengine angekuja kuachia madaraka, lakini alikuwa ameshafuata mfumo wa nchi nyingi za kiarabu wa kurithishana madaraka kwa watoto ama ndugu. Inasemekana alikuwa amemuandaa mtoto wake mmoja wa kiume kuja kurithi madaraka.
Pia tatizo jingine ni labda kukamatwa na kufunguliwa mashtaka endapo serikali itakayoingia madarakani itakuwa na uhusiano wa karibu na mataifa ya magharibi, kumbuka walikuwa wakimuwinda sana.
Nina Imani kwamba Ghaddafi alikuwa na mawazo ambayo ni mabaya sana kwa mataifa makubwa na mazuri sana kwa walibya. Alikuwa tatizo kwa mataifa hayo na si kwa taifa lake.