figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 27,813
- 63,269
figganigga,
..hapa kuna mambo mawili.
..1. kuna bias ya UN dhidi ya wa-Congo. Huwa hawaweki mashinikizo kama hayo kwa askari wa Rwanda wenye tuhuma za mauaji ya kimbari. Tena askari hao wamepata kupewa nafasi ya kutumikia katika vikosi vya UN.
..2.Kabila hataki kuwapiga FDLR kwasababu walimsaidia ilipovamiwa na Rwanda. Pia Rwanda imewapa hifadhi wapiganaji wa M23, sasa Kabila naye analazimika kuwa na kundi lake linalompa leverage dhidi ya Rwanda.
cc jMali, Jasusi
chanzo cha habari ni AFP, i wonder nani hasa kaandika hii habari.
1. "The senior UN peacekeeping official, who spoke on condition of anonymity,"
hivi toka lini UN ikatoa agizo zito kama hilo kupitia anonymous official?
2. JokaKuu ni kweli kabisa kuhusu double standards za UN. cheki huyu jamaa aliteuliwa kabisa na UN akiwa na tuhuma nzito zenye uthibitisho. Na pia kila UN ikitaka kutoa ripoti hasi kuhusu kagame, kagame anatishiaga kutoa majeshi yake kwenye operesheni za UN mfano darfur, UN badala ya kuchagua nchi nyingine yenyewe inakubali matakwa ya kagame na kuzikalia ripoti.
Rwandan General Accused of Supervising Death Squad Leaves UN | Foreign Policy Journal
3. Mi nadhani kama hii kauli ni kweli: "or else the United Nations will withdraw its support for the operation." basi poa, kabila anatakiwa ku-stick to his guns, ili UN wajitoe (Tanzania included), halafu FDLR wabakie kama kawa, kama ambavyo M23, Ntaganda na watuhumiwa wenzie wa mauaji ya DRC wanavyohifadhiwa Rwanda na uganda.
Kagame aliunda kundi la m23 ili kuwapiga FDLR sema wakapitiliza malengo yao, wakataka kutawala. FDLR wanasema wanataka mazungumzo na Rwanda kuhusu usalama wao lakini kKagame kakataa kwa madai kwamba ni watuhumiwa wa mauaji ya kimbali mwaka 1994 miaka 20 iliyopita. Wale FDLR walikua Askari wa Habyalimana aliyekufa kwenye ajali ya ndege ambayo wanasema Kagame ndo aliitungua. Kama wakiwachokoza basi Rwanda haitakua na aman nahisi kwa sababu itabidi wajichimbie kwenye mapoli ya Rwanda.
Hata hivo jana manisikia majeshi ya Kabila yameanza kuwavulumishia makombola hao waasi wa FDLR lakini UN bado haijaanza. Hiyo inaweza kuwa ni janja ya Kabila, atakua kashawahamisha sababu walimsaidia sana.
Kupigwa kwa FDLR itakua sherehe kwa Kagame.
figganigga,
..2.Kabila hataki kuwapiga FDLR kwasababu walimsaidia ilipovamiwa na
Rwanda. Pia Rwanda imewapa hifadhi wapiganaji wa M23, sasa Kabila naye
analazimika kuwa na kundi lake linalompa leverage dhidi ya Rwanda.
cc jMali, Jasusi