Ndugu umesema kweli ila kumbuka hata familia zetu yaani mke na watoto wakisikia tu baba unataka kuacha kazi na ujikite kwenye ujasiriamali basi wasiwasi unatanda nyumba nzima, je tutaishije? unajaribu kuwaondolea wasiwasi na njisi kipato kitakavyokuwa lakini bado wasiwasi unatanda sababu wanaona income haina uhakika (security) hasa wa mama ndiyo waoga numberi one.
Wazazi, ndugu ya jamaa (hasa kama unatoka ukoo usio na wajasiriamali) ni waoga kupindukia, wengine inafikia unawekwa baraza kwa nini unataka kuacha kazi? umeingiwa na mapepo gani kijana wetu?
Sasa mambo kama hayo lazima uwe na msimamo mkali sana vinginenvyo utaishia kuajiriwa hadi kiinua mgongo unapofikia miaka 60, unapewa NSSF yako kidogo ndiyo unajengea kibanda, na kwa wale wa serikalini unapewa kiinua mgogo kidogo na pensheni ya elfu hamsini kwa mwezi.
Uthubutu ndiyo tatizo kuu na tatizo la jamii yetu sababu tangu zamani hatukuwa na utaratibu wa kujitegemea, watu tulisoma huku mawazo yetu yote yakiwa katika kupata ajira either serikalini au mashirika ya umma at that time.
Thanks GOD sasa hivi vijana wa 25 and less wanajua suala zima la dhana hii ya ujasiliamani, sisi tuliosoma enzi ya mwalimu ambao ni zaidi ya 35 and above ndiyo hasa wenye tatizo hili.