Umechoka kutumwa, ujasiriamali unautaka lakini bado Muoga? Ushauri ....

Kweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,151
1,500
Linapokuja suala la kuingia kwenye Ujasiriamali wengi wetu tuna kawoga na hatupendi kujaribu lakini jee usipojaribu utawezaje?
Wengine wetu bado tuna mindset ya kuajiriwa, wako tunaosubiri wakati muafaka na biashara ya uhakika, wengine tunaogopa kufilisika na majanga mengine. Kwaufupi tume-base sana kwenye negative mindset.
Mjasiriamali anatakiwa awe MJASIRI na asiyeogopa , wale wajasiriamali wazoefu wanajua kwamba "biashara haikupatii mafanikio bali wewe kwa juhudi zako ndio unaifanikisha biashara"

Kwa kupata mwamko zaidi soma hapa: How to Overcome Startup Fears
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,648
2,000
Ndugu umesema kweli ila kumbuka hata familia zetu yaani mke na watoto wakisikia tu baba unataka kuacha kazi na ujikite kwenye ujasiriamali basi wasiwasi unatanda nyumba nzima, je tutaishije? unajaribu kuwaondolea wasiwasi na njisi kipato kitakavyokuwa lakini bado wasiwasi unatanda sababu wanaona income haina uhakika (security) hasa wa mama ndiyo waoga numberi one.

Wazazi, ndugu ya jamaa (hasa kama unatoka ukoo usio na wajasiriamali) ni waoga kupindukia, wengine inafikia unawekwa baraza kwa nini unataka kuacha kazi? umeingiwa na mapepo gani kijana wetu?

Sasa mambo kama hayo lazima uwe na msimamo mkali sana vinginenvyo utaishia kuajiriwa hadi kiinua mgongo unapofikia miaka 60, unapewa NSSF yako kidogo ndiyo unajengea kibanda, na kwa wale wa serikalini unapewa kiinua mgogo kidogo na pensheni ya elfu hamsini kwa mwezi.

Uthubutu ndiyo tatizo kuu na tatizo la jamii yetu sababu tangu zamani hatukuwa na utaratibu wa kujitegemea, watu tulisoma huku mawazo yetu yote yakiwa katika kupata ajira either serikalini au mashirika ya umma at that time.

Thanks GOD sasa hivi vijana wa 25 and less wanajua suala zima la dhana hii ya ujasiliamani, sisi tuliosoma enzi ya mwalimu ambao ni zaidi ya 35 and above ndiyo hasa wenye tatizo hili.
 
Kweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,151
1,500
Ndugu umesema kweli ila kumbuka hata familia zetu yaani mke na watoto wakisikia tu baba unataka kuacha kazi na ujikite kwenye ujasiriamali basi wasiwasi unatanda nyumba nzima, je tutaishije? unajaribu kuwaondolea wasiwasi na njisi kipato kitakavyokuwa lakini bado wasiwasi unatanda sababu wanaona income haina uhakika (security) hasa wa mama ndiyo waoga numberi one.
Hii transition kutoka kwenye kuajiriwa na kuingia kwenye kujiajiri ndio ngumu sana na inataka uwe makini sana, inabidi uende hatua kwa hatua , unaaza kufanya research ya kutosha kwa business idea yako wakati wewe bado ni muajiriwa, ukiridhika nayo unaandaa matayarisho yote, ofisi, vitendea kazi, mtaji nk. haya yote unayafanya wakati bado umeajiriwa, baadae unachukua likizo ya muda mrefu kama miezi 6, ndipo unaanza project yako, baada ya miezi hiyo sita bila shaka utakuwa na idea kama ujasiriamali unakufaa ama urudi kazini, angalizo ni kwamba kwa wale wanaoanza mwaka wa kwanza mara nyingi huwa unasoma (learn the trade) kwa hio hata kama kuna hasara ama faida ndogo katika hio miezi 6 usikate tamaa, rekebisha wapi unaona ulikosea.

Uthubutu ndiyo tatizo kuu na tatizo la jamii yetu sababu tangu zamani hatukuwa na utaratibu wa kujitegemea, watu tulisoma huku mawazo yetu yote yakiwa katika kupata ajira either serikalini au mashirika ya umma at that time.
Hilo ndio neno "uthubutu"

Thanks GOD sasa hivi vijana wa 25 and less wanajua suala zima la dhana hii ya ujasiliamani, sisi tuliosoma enzi ya mwalimu ambao ni zaidi ya 35 and above ndiyo hasa wenye tatizo hili.
Tanzania ni katika nchi chache hivi sasa ambayo ina opportunities nyingi za ujasiriamali, na hili wageni wengi wameligundua, tatizo wanashindwa na vibali na regulations zetu lakini sisi wenyewe ambao tuna mwanya wa kuzitumia nafasi hizi bado tuko na usingizi .
 
Erick_Otieno

JF-Expert Member
Mar 28, 2010
626
1,000
Ujasiriamali naufananisha na kujitoa muanga yaani kujilipua......Ukishaingia sahau habari za kurudi nyuma kuajiriwa. Ndio, kuna changamoto nyingi sana unapoanza na hii ni hatari sana kama utaingia kwa mtindo wa kujaribisha. Wakati mwingine inaweza kuchukua hata miaka kadhaa kabla ya kupata mafanikio unayoyatarajia. Nilikutana na marehemu Mzee Elvis Musiba (R.I.P) kwenye moja ya networking za ujasiriamali, na moja shuhuda za maisha yake kibiashara alisema alishawahi kufilisika kabisa mara mbili. Hata hivyo, naamini maisha ya amani na uhuru ni ya kijasiriamali, mafanikio ni matokeo...
 
  • Thanks
Reactions: LAT

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom