Umbali umenifupishia mapenzi

msingi pesa

New Member
Joined
May 16, 2018
Posts
1
Reaction score
1
Wasalamu wote,

Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada yangu.

Miaka 4 iliopita nakumbuka bado nikiwa shuleni, kidato cha nne katika shule moja iliokuwepo jijini dar es salam. Nilibahatika kupata demu mmoja mkali wa kiarabu, mtoto alikua mkali sana.

Mimi mwenyewe nilimpata kibahati pale ambapo tulipo pangwa kufanya Project ya watu 10. Kama unavojua mzee kishule shule, nilikua muchknower so ilikua aesy tu kutema madini kwa huyu malkia.

Nashukuru mtoto alinielewa mzee nikakamata chombo.Mahusiano yetu yalienda mpaka pale ambapo tulimaliza shule na Post za kwenda form 5 kutoka.. Nika muaga bibie mzee na kwenda mkoa ambako shule niliopangiwa iliko.

Kwa bahati mbaya shuleni kule cm hazikulusiwa kwaio nikapoteza mawasiliano nae pindi niko huko na mimi sikurudi likizo muda wote wa miaka miwili kwani niliishia kwa baba yangu mkubwa aliekuako karibu na shule hio.

Sasa baada ya kumaliza elimu ya advance nikarudi Dar es Salam kwa ajili ya kujiandaa na masomo ya chuo. Nakumbuka siku moja nilipata mwaliko wa rafiki yangu mmoja ambae nilimaliza nae form 4 kwenye sherehe yake ya harusi Looh! Sikutegemea kukutana tena na binti mzuri alievutia misili ya malaika nilifarijika sana.

Baada ya hapo nikapata muda wa kuongea nae nikapata namba mpya baada ya kupoteana mda wa miaka miwili. Nilivorudi nyumbani nikawa nachati nae but respond yake ilikua ndogo sana maana some time anatumia hata lisaa lizima kama interval ya kujibu text nilifikiri kwamba sasa moyo wake haupo tena nami.

But niliwaza moyoni kwamba kama angekua hanipendi asingejibu text kabisa. Nikajiridhisha na hio hali sababu nampenda lakini mambo ndo yanazidi. Mpaka sasa nikawa najidharau sijui kubembeleza nini mbona wengine wanateleza ila kwangu ni ugumu tuu.

Ila ivi juzi nimepigia simu kama mara 10 hapokei. Meseji kama zote kimya. Kweli kupendwa ni ajira sina vyeti yani sielewi jamani msaada wa mawazo mniokoe kijana mwenzenu.
 
Kuna mtu hapa Bar kafanya "shambulio la AIBU" kakohoa na kubanja kabisa mbele ya muhudumu.. Huyu ni miaka mitatu itamkuta na faini juu..
 
Kwa hiyo ulitaka miaka miwili yote demu asiliwe eti akae anakusubiri wewe uliyeenda kusoma kantalamba
 
Ok sawa, kwahiyo msaada gani unahitaji kwetu? Labda nipe namba zake, nimjaribu na mimi akipokea nitamwambia apokee simu yako.
 
acha kuhangaika na asiekupenda maana atakupa jeraha la mahaba uchukie dada zetu bure!,kupendwa ni moja ya furaha iletayo amani na utulivu hivyo basi hufanya hata mambo yako kwenda fresh.. Maana hakupi stress.
Hata hivyo nisikuvunje tamaa yako,anza kutumia akili kumrudisha akupende gharama za muda,pesa na kufikiri zitakutoka kidogo!.. Muonyeshe kwamba we ni watofauti lkn tofauti hiyo inahitaji kumsoma saikolojia yake ili ufanye maamuzi ya nini ufanye! He he play your part.
 
Pole sana, endelea na mambo mengine wadada wapo tu.
 
Mkuu inabidi uelewe people change, the girl uliemuacha kipindi kile sio wa leo, so usitegemee hisia zake bado zitakuwa zilezile n.k

Be glad uliweza kukutana nae tena, lakini hiyo ya kusema sijui unataka kurudisha penzi, so far unaona kabisa dalili ni mbaya kuhusu hiyo. We accept and move on.
 
Hapo ndio huwa mnakosea; baada ya kuipata namba yake, jambo la kwanza ulitakiwa umfanyie muamala wa M - Pesa au Tigo Pesa halafu mambo mengine yaendelee.
 
sina cha kukushauri mkuu,

huyo hakupendi there is no way unaweza mrudisha akupende.

unaweza rudia matapishi ata kama ni yako?

kama jibu ni HAPANA bhasiii tafuta mwingine mkuu Moyo haupendagi mala mbili mtu mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…