Ulitegemea kipenga alichopoteza refa kitoke wapi uwanjani?

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
1,884
Reaction score
1,466
Ulitegemea kipenga na kadi alivyopoteza refa vitoke wapi?
Mpambano unaendelea. Katikati ya mchezo,refa
anagundua kuwa amepoteza kadi-ya njano na
nyekundu pamoja na filimbi. Kutokana na kasi ya
mchezo, anauchuna. Haisikiki filimbi wala
haionekani kadi hata pale inapohitajika.
Wachezaji wanakatana mitama ya kiama lakini
kimya. Wachezaji wanatukana na vikumbo kupigana
lakini kimya. Mpira unatoka na kurushwa tena bila
filimbi kupigwa.
Wachafu wanacheza rafu na wasafi wanachafuliwa.
Wachezaji wanatamba kila namba na kujigamba.
Refarii yuko kimya huku akionekana dhahiri shahiri
kuwa kasi ya mchezo inamshida.
Anajikaza kisabuni tu. Anaendelea kukimbia hapa na
pale akiomba tu mchezo uishe salama. Itasikika
filimbi gani goli likifungwa? Atasemaje kuwa ni goli
halali au haramu? Mpambano hauna mfano.
Refarii anafanya siri. Hasemi ukweli kama
amepoteza filimbi na kadi. Anakufa na tai yake
shingoni. Hata mchezaji kibaka naye kajichanganya
mpirani na anakaribia kutangazwa 'man of the
match'.
 
Naomba kujua mpaka saaa hii nikipindi Cha Kwanza au Cha pili Cha mchezo?
 
Siyo kila andishi litaeleweka...

Kuna ile unadhani umeandika fasihi kumbe pumba.
 
Ha ha ha haaaaaaaaa,ukiangalia jamii nyingi ambazo zinawabobezi na manguli wa fasihi nizile ambazo zimepitia mapito ya mpito
 
Team captains watimu zote mbili wanatazamana wasijue lakufanya. Wanabaki kuwasihi wachezaji wenzao wapunguze rafu lakini haisaidii. Wameshagundua udhaifu wa mwamuzi wa mchezo. Wanakaa kimya kungoja dakika 90 ziishe.

Kuna timu inajaribu kufanya mabadiliko ya mchezaji lakini wachezaji wa akiba wanaonekana kuwa dhaifu kuliko walio uwanjani. Hata hivyo watafanyaje kama mwamuzi kadondosha kipenga!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…