Ukwepaji kodi kariakoo!

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Awali napenda kuishukuru serikali kwa kuweka wapelelezi wao kwenye maduka kariakoo.
ili kuwabaini watu wasiotoa risiti za EFD. Na wale wanao ondoka bila risiti baada ya kununua bidhaa zao hili ni jambo jema, Lakini ukwepaji kodi mkubwa karikakoo hauko katika kutokutoa risiti za EFD tu..
ukwepaji unafanyika kwa kutoa risiti yenye thamani pungufu kwa mzigo ulionunuliwa mfano umenunua mzigo wenye thamani ya tsh 600,000 au Tsh 1,000,000 muuzaji atatoa risiti ya tsh 2,00,000 au hata Tsh150,000 ukiuliza anakujibu brother hiyo si ya njiani tu?
Ukikomaa kutaka risiti kamili unakuwa umetengeneza uadui kesho ukija inakuwa ngumu sana kuhudumiwa kwenye duka hilo..!!
Ushauri wangu,
TRA waendelee na hiyo system ya kuvizia kwenye maduka lakini awamu hii wakamate wanunuzi waulize bei ya mizigo waliyonunua kisha waangalie risiti walizo nazo kama zina thamani ya mzigo iliyobebwa.! Wapige thamani ya mzigo na risiti walizo nazo..!
wakifanya hivi kwa mwezi mmoja naamini kila mnunuzi atakuwa makini.
mwisho watu wao wanaowaweka sokoni kariakoo wanatambulika na wafanyabiashara wenye maduka kuwa ni watumishi wa TRA hivyo ni vema ama wakawa wakibadirisha mara kwa mara.
nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adhabu iwe 20 times thamani ya bidhaa sema hii isiwe loophole ya vitendo vya rushwa kwa TRA. Afisa wa TRA atakaekamatwa Na rushwa adhabu owe 40 times ya thamani ya mzigo
 
hapo kwenye kulinganisha thamani ya kitu na kilichoandikwa kwenye risiti mh cjakuelewa na itajua ni usumbufu sasa kuanza kubishana na tra kua sijanunua bei

bei ilioandikwa kwenye risiti ndo niliyonunulia mzigo bas!! tusilazimishane kua sijanunua ivyo

yule anaeuza kila mteja anakua na bei yake inategemea jinsi alivyokushawishi mpaka ukakubali kufikia bei yake kiufupi maswala ya bei ni yangu na ya alieniuzia basi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanyooka tu.Tulizoea sana kupata faida bila ya kulipa kodi
Ajabu ya hawa wafanyabiashara,mtu yupo tayari kulipia pango kwa mwezi milioni 3,anatoa kodi ya mwaka mpaka miaka miwili,lakini hataki kuilipa TRA
 
Mkuu nadhani hapa ni maumivu na uzalendo tunaofanya mahali kwingine halafu kuna mtu kirahisi rahisi tu anakwepa kodi na ukimuelewesha anakuletea jeuri "kama hutaki acha mzigo"!
Anaekamatwa amekubali risiti pungufu dawa yake ni ndogo alipe mara 20 zaidi.wakifanya hivi hata kwa miezi mitatu mfululizo nina hakika huu upuuzi utaisha tu.
kabla hawajathibitisha na kuoanisha bei iliyopo kwenye risiti yako TRA (Mtu) anakwenda kwenye duka hilo hilo na kuuliza bei ya bidhaa ileile pasipo mwenye duka kujua then inalinganishwa na idadi uliyokamatwa nayo na risiti uliyo nayo mkononi..
kama zinaendana hapana shaka lakini kama wakigundua kuna mapungufu au ukwepaji kodi.
wewe uliepokea risiti na aliyetoa risiti wote muwajibike. Kwa makosa mliyofanya ya kukwepa kodi ya serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…