Nilitaka kusema, wengi wenu hapa inaonekana mmezaliwa hivi karibuni.
Kwa wale wahenga nadhani mnakumbuka enzi za mieleka hapa Tanzani.
Kwa sasa mieleka imeshindwa kuchezwa kwakuwa Bodi ya mieleka imeshindwa kutimiza masharti ya mieleka kama kuwa na jukwaa maalum, ambalo ni ghali sana na jukwaa la mieleka moja linafikia thamani ya Tsh, zaidi ya Bilioni moja.
Wakati ule wa mieleka akina Power Bernado. Power Mwanza. Power Chaka. Power Vurumroma, Power Mabura walikuwa wanacheza Mieleka ya Ukweli hapa Tanzania.
Viti vilikuwa vinatumika lakini sio kila kiti, ni viti maalum vya kupigania. Ukiangalia WWE utaona viti vyao wanavyo pigania vinafanana na sio kila kiti.
Katika mapambano ya Mieleka kuna mapambano ya kutumia silaha maalum, zinapitishwa kutumika kama Meza Viti, Rada yaani ngazi nk, na kuna aina ya upigaji wake, hata ile nyundo anayetumia mpinzani wa Underteker (nimemsahau jina) ina aina yake ya utumiaji, ndio maana huioni ikitumika kumtwanga nayo mtu kichwani au kwenye uti wa mgongo.
Kuna mapambano hayatakiwi kutumia silaha, na kuna mapambano hayatakiwi kuingiliwa, wachezaji wanacheza ndani ya wavu wa chuma.
Maana kuna wakati fulani ilikuwa mkicheza pambano na kama kuna mtu kaingilia kumpiga mchezaji X, basi Mchezaji Y anapewa ushindi.
Lakini wajanja wakaingiza hila ya kwamba adui wa mchezaji X anaingilia pambano na kumpiga mchezaji Y ili mchezaji X anyang'anywe ushindi.
Hivyo WWE ikaaamua kuwafunika wachezaji kwenye wavu wa chuma kama wanataka mshindi apatikane bila kusaidiwa na mchezaji mwingine.
MAIGIZO KATIKA MIELEKA.
Kuna kuigiza ndani ya mieleka lakini maigizo yale yanakuwa wakati wa kupanga pambano fulani ili kuvutia mashabiki, kwa mfano.
John Cena anataka kucheza na Rand Orton pambano la ukweli.
Ili kunogesha pambano John Cena ataandaliwa pambano na Rey Masterio, pambalo ambalo linakuwa la ushindani kama kawaida na mshindi atachukua zawadi yaani fedha kama kawaida.
Katikati ya pambano Cena bila kijua, Rand Orton ataingilia Pambano kumpiga John Cena na kumsaidia Ray kushinda pambano hilo, hivyo kuamsha hasira kwa Cena kutaka kulipa kisasi kwa Rand Orton, hapo sasa Pambano halisi linaandaliwa kati ya Cena na Orton.
Mfano hakisi ni pale WWE ilipotaka kuwapambanisha wacheaji ndugu Mart na Jeff hard.
Jeff alikuwa anagoma kucheza na ndugu yake lakini pesa nyingi iliyoandaliwa na WWE ambayo ilimvutia Mart na kutaka kumlazimisha Jeff akubali kupigana naye ili wavute ule mkwanja ama yeye Mart au ndugu yake Jeff.
Hivyo WWE wakafanya Njama kwa kumshirikisha Mart, wakaanda pambano kati ya Jeff na mchezaji mwingine, Jeff akiwa hana habari, katikati ya mchezo ambao Jeff alikalibia kushinda Mart akaingilia kati, akampiga Jeff na kumtolea maneno mengi ya kashfa hadi Jeff akakasirika na kukubali kucheza na kaka yake Mart hard, na wakacheza pambano ambalo liliingiza pesa nyingi kwakuwa liliandaliwa kwa jinsi hiyo, Mart mbaye ni yule kama anachechemea alishinda pambano.
Mieleka ni mchezo halisi ila unambwebwe wakati fulani ili kuhamasisha washabiki na kuingiza pesa nyingi
UHALISIA
Mzungu au mtu mwingine hawezi kupoteza muda wa kwenda kupoteza pesa yake kuangalia utapeli wa michezo wa watu mahali fulani.
Michezo ni kitu halisi, kama Komedi inaandikwa kabisa hii ni Komedi. Kama Bongo Muvi itawajulisha watazamaji wake kuwa hii ni Bongo Muvi.
Na wakati ule wa mieleka ya hapa Tanzania mimi nilikuwa naenda kuangalia na ilikuwa inacheza sawasawa na tunavyoona leo katika WWE, Viti vilitumika pia tena ni vilevile vya WWE, sema sasa hivi wenzetu wameboresha mambo mengi sana.
Kama kuna waliowahi kucheza mieleka, wapo humu JF wanaweza kututhibitishia zaidi ukweli huu.
Kukosolewa kunaruhusiwa.
Mkuu umeandika ukweli kabisa lakini kuna issue moja hujaijua.. hiyo issue ni kwamba wale jamaa hawapigani kabisa mfano orton vs cena pale hamna anayempiga mwenzie hata kidogo labda kwa bahati mbaya, zile ngumi mateke ni brush tu hazimfikii mtu zile zinarushwa kijanja sana . Chunguza hilo ingia you tube angalia hawa jamaa wame fool watu kibao kwa mda mrefu