Wazee wangu nchi hii tuna kila kitu isipokuwa tunachokosa ni kimoja tu uongozi bora na siasa safi.Tatizo hapa ni watawala ambao bila shaka ni ccm.Watawala hawa kwa miaka 50 wamekosa dira ya kuingoza nchi hii kuelekea kufaidi neema tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.Wamekuwa ni wabinafsi, wamekosa uadilifu,sio wazalendo,wamekosa pia akili na uelewa wa masuala ya uchumi na hivyo kuachia raslimali za nchi hii kuchukuliwa na wageni bila huruma huku wao wakipewa kitu kidogo sana kwa ajili yao na famiilia zao.Tuache masihara ya kiitikadi ktk masuala nyeti kama haya.Ndugu zangu angalieni mfano wa vinchi vidogo kama Mauritius hawana rasilimali yeyote ni kisiwa kidogo ktk bahari ya Hindi,wanategemea utalii na kilimo cha miwa pekee,angalia walivyopiga hatua.Wana uchumi mzuri,ni mojawapo ya nchi pekee nne Africa zenye uchumi mzuri sana zingine ni Botswana,Gabon na Africa ya Kusini wana literacy rate 85% na ni moja ya nchi zenye utawala bora na democracy nzuri,wamewahi kupata nishani ya Ibrahim kuhusu utawala bora.Sasa sisi tuna tatizo gani hadi tuwe masikini kiasi hiki licha ya rasilimali lukuki na ardhi nzuri tuliyo nayo.
Tujiulize wananchi tunahitaji kuchukua hatua,na hatua nzuri kwa sasa ni kubadilisha uongozi wa nchi kabisa tuwaone na wengine watafanya nini badala ya kutegemea walewale ambao wametuangusha kwa muda wote huo.Mbona nchi za wenzetu hubadilisha utawala mara kwa mara na wanaendelea mbele,sisi tunaogopa nini?Ni wakati muafaka wa kubadilisha watawala kwani hata wengine wakifanya vibaya si tutawaondoa tu shaka ya nini?
huwi mpumbavu kwa kuitwa,ni sifa uliyonayo,hata usipoitwa utabaki hivyo!
Wana-JF, napenda kuwashirikisha alichosema Mzee Peter Kisumo kuhusu CHADEMA:
‘Tatizo kubwa kwenye Chadema kuna wanaharakati na si wanasiasa, na haiwezekani kuongoza serikali kwa kuwa na viongozi wanaharakati'.
"Hawa Chadema wanachokifanya ni kuvizia makosa madogo madogo ya serikali na kisha kuwashawishi wananchi wawe upande wao,".
"Wapo viongozi wa Chadema na waasisi, kama Mzee Edwin Mtei na watu wengine makini ninaowafahamu ndani ya chama hicho, sijawahi kuwasikia wakiropoka hovyo kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa chama hicho."
'Ikiwa hulka hiyo itandelea, kuna hatari ya kukosa sifa ya kushika dola vinginevyo watapata shida, kwani hakuna serikali inayoweza kwenda kwa kuendeshwa na wanaharakati'.
'Inatakiwa chama ambacho kitashinda kiwe na uwezo wa kuongoza katika hali ya amani na utulivu na si kuingia kwenye machafuko mara baada ya uchaguzi'.
'Ili Chadema ishike dola, ni lazima wajitahidi kujenga safu ya uongozi wa kutawala na si kuwa na viongozi ambao kila wakati wanahamasisha watu kuandamana, kugoma na kuvizia makosa ya serikali iliyopo madarakani'.
'Wanachokifanya Chadema ni sawa na wawindaji wanaokoka moto kwa ajili ya kuchoma nyama ili hali nyama yenyewe hawajaipata, ..... kazi ya kuing'oa CCM si rahisi kama inavyofikirika'.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Mkuu umesema kweli ila hawa washabiki wa CHADEMA wamekuwa vipofu hata hawataki kufukiria japo kidogo. Je CHADEMA ni kipi wanachofanya? Zaidi ya kulalamika kila wakati na kuwadanganya wananchi hukuwakiwajaza jazba ambayo matokeo yake ni machafuko.
Ninaamini tunaweza kujadili bila ya kuitana wapumbavu.
Kwa hiyo wanasiasa ni akina nani, Lusinde, Nape au wassira???Haya maneno hayawezi kueleweka kwa hawa vijana wa cdm wasiojua siasa. Ukweli ndio huo, chadema ni wanaharakati na si wanasiasa.
Wana-JF, napenda kuwashirikisha alichosema Mzee Peter Kisumo kuhusu CHADEMA:
Tatizo kubwa kwenye Chadema kuna wanaharakati na si wanasiasa, na haiwezekani kuongoza serikali kwa kuwa na viongozi wanaharakati.
Hawa Chadema wanachokifanya ni kuvizia makosa madogo madogo ya serikali na kisha kuwashawishi wananchi wawe upande wao,.
Wapo viongozi wa Chadema na waasisi, kama Mzee Edwin Mtei na watu wengine makini ninaowafahamu ndani ya chama hicho, sijawahi kuwasikia wakiropoka hovyo kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa chama hicho.
'Ikiwa hulka hiyo itandelea, kuna hatari ya kukosa sifa ya kushika dola vinginevyo watapata shida, kwani hakuna serikali inayoweza kwenda kwa kuendeshwa na wanaharakati'.
'Inatakiwa chama ambacho kitashinda kiwe na uwezo wa kuongoza katika hali ya amani na utulivu na si kuingia kwenye machafuko mara baada ya uchaguzi'.
'Ili Chadema ishike dola, ni lazima wajitahidi kujenga safu ya uongozi wa kutawala na si kuwa na viongozi ambao kila wakati wanahamasisha watu kuandamana, kugoma na kuvizia makosa ya serikali iliyopo madarakani'.
'Wanachokifanya Chadema ni sawa na wawindaji wanaokoka moto kwa ajili ya kuchoma nyama ili hali nyama yenyewe hawajaipata, ..... kazi ya kuingoa CCM si rahisi kama inavyofikirika'.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Kama mtu anasifa zote za upumbavu tumuiteje?Kama mzee anadhani chama cha upinzani kipo kukipamba chama tawala kinaposhindwa kuimarisha serikali yake na kuanza kulialia mzee huyo tumuiteje? Kama serikali ina subiri fedha za wanywa pombe na wavuta sigara huku madini yake yakichukuliwa kuwa neemesha wageni tuiiteje?Ninaamini tunaweza kujadili bila ya kuitana wapumbavu.
Sasa kwa kauri kama hii ukiitwa mpumbavu utakasirika? Nenda kamuulize msajiri wa vyama akufafanulie swala hili. La si hivyo wewe na huyu kibabu wako wote ni wapumbavu wachumia tumbo!Mabadiliko ya uongozi wa nchi yatafanywa na Watanzania kidemokrasia watakapoona kuna haja ya kufanya hivyo na muhimu zaidi watakapoona kuna chama kinachoweza kuaminika kukabidhiwa dola.
Kwa sasa hakuna chama makini cha upinzani kinachoweza kuaminika na kupewa ridhaa hiyo. Waliopo ni wanaharakati tu.