Kwa ukimwi, tatizo ni jamii yetu inavyouchukuliwa huu ugonjwa, unaonekana kama mtu akiwa nao ni mzinzi, mzembe, hafai nk. Sasa kwa kuuona hivyo, kumwambia mtu ana ukimwi ni kumuonesha mabaya yote yanayoambatanishwa na ugonjwa wenyewe. Kumbe mtu anaweza kuupata bila kufanya ngono (lakini ngono ndio inachangia kwa asilimia kubwa sana). Sasa huyu itabidi akapimwe, kama anao ataambiwa alimnyanyapaa mgonjwa wa ukimwi, kama hana atashitakiwa na kosa la kumwambia ana ukimwi wakati hana, pia atashitakiwa kwa kosa la kumzushia kuwa anachukua wame za watu.