UKAWA waiteka CC ya CCM


Kwa hiyo Sitta ni mwenyekiti wa bunge la katiba asiye huru.Anafuata matakwa ya Nape
 
Katiba mpya ni kitanzi cha CCM hawawezi kukwepa kinachosubiriwa ni muda tu watachenga lakini mwisho wake wataingia wenyewe kama ilivyokuwa suala la vyama vingi.
 
Hawakutaka kuwapa elimu ya uraia Watanzania ili wasiijue Nchi yao, Historia yao, Miiko yao, Ndugu zao, sasa Ukawa fanyeni hiyo kazi lazima wazivae suruali vichwani, hawakuwa na majaribu na maswali magumu ndio maana tukichagua Mbunge mwembamba baada ya mwaka anapata kitambi hawakuwa na changamotoooooooo wacha sasa, Nawashauri ukawa watoe elimu kwa wananchi kujua haki zao ingawaje wenyewe wanaita mnawapotosha wananchi, Msirudi bunge la katiba kama wataendelea kujadili vitu ambavyo havipo kwenye rasimu, wameanza na muundo wa Serikali nawaambia wakimaliza hapo na yale ya mbunge kugombea misim miwili tu wataikataa, kuwa na waziri 15 watakataa, sababu Rais alisha vijadiri hivyo na kuviponda kama mnakumbuka kazi bado kubwa maana wabunge wa CCM ni bendera tu.
 
warudi kula matapishi yao, kweli itakuwa hatari, wataficha wapi sura zao wale waliojiapiza, ngoja tusubiri mwisho wa hii muvi tuone stering ccm akifa.
 
Kwani CCM ni nini vile? Ni binadamu? Mnyama? Au jini? Niambieni nifahamu.
 
Ccm kukubaliana na maoni ya wananchi na Ukawa ndio kete ya mwisho ambayo ataitoa yule yule kigeu geu ambaye hugeuka wenzake pindi wanapokubaliana ndugu Jk.
 
Lakini mbona m/kiti wao aliwaambia wajiandae kisaikolojia!inamaana hawakumwelewa?
 
CCM wamekwisha sema kuachana na msimamo wa serikali mbili ni ndoto, wako tayari waingie msituni...kuisambaratisha nchi.
Njia nyingine ni kuwarubuni wabunge wa upinzani kwa kuwahonga milioni makumi kadhaa wakati huu kabla ya bunge la katiba ili wapunguze munkari na kuamua kurudi bungeni Agosti. Kwa lugha nyepesi ya kichama ni kuwapa takrima kila mmoja wao. Si unajua takrima kwa ccm ni ruksa?
 
Watabadilisha iwe 2/3 ya wajumbe wote jumla, badala ya 2/3 ya wabara na 2/3 ya wa visiwani kama inavyotakiwa.
 
Kama wako tayari kuingia msituni aisee, that's good; Mungu anaweza akawageuza wakawa nyani na kutokomea hukohuko!
Ngoja tumuombe Mungu awaharakishe kukimbilia msituni!

Mimi siku John Komba akiingia tu mstuni kama alivyodai, lazima niingie nae! Ule mgongo jamani. Huku uraiani sheria zinawalinda sana, lakini kule msituni mtu unamtatua marinda kirahisìiiìi!!!!
 

CCM hawana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…