Hakuna dalili zozote zinazoashiria kupata katiba mpya ambayo Watanzania wenyewe wamekuwa na hamu yakuwa nayo kwa kushiriki wenyewe katika kutoa maoni yao katika tume iliyoundwa na serikali (TUME YA WARIOBA) maoni ambayo kwa ujumla wake sasa hayaheshimiwi yanapuuzwa na watu wachache kwa maslah yao wenyewe....Watu hawa wachache wanajifanya wana akili nyingi kuliko Watanzania wengine wote,Wanadhani wao ni wajuaji zaidi kuliko Wanatume ya Jaji Warioba na wenzake walioizunguka nchi nzima na kukusanya kile wananchi wanachokihitaji,Wanajitia uchizi.
Ukawa mna kila sababu ya kutupa kile ambacho wananchi tunakitaka kulingana na wakati wetu wa sasa ulivyo...Tunaomba mtupe Katiba mpya kwa gharama yoyote,Tunaamini si rahisi ccm kukubali kutupa katiba inayotokana na rasimu ya Warioba kwasababu wakiruhusu hilo watakuwa wameziba masilah yao wao kama ccm na si kama Watanzania, wanajua madhara yatakayowakuta baada ya kuanzishwa kwa serikali ya tatu(TANGANYIKA HURU) Lakini madhara hayo kama yatawakuta hawa hawa wapinga Maoni ya wananchi tunaamini utakuwa ndio mwanzo wa kasi ya kweli katika ujenzi wa Taifa imara....Tunatamani kuiona katiba mpya itakayoruhusu mikataba mbalimbali ya kifisadi kufumuliwa hasa ile inayowaruhusu wawekezaji kuwekeza katika maliasili na ardhi yetu kwa zaidi ya miaka mia moja tunajua wanaccm ni ngumu kutupa katiba ya namna hii.
Tupo nanyi bega kwa bega wana Ukawa,Tunahitaji kusikia mkitushirikisha pale mtakapoona nguvu ya uma inahitajika,Bungeni mlikuwa wachache lakini huku nje ndugu zenu wa Tanzania tupo mamilioni kwa mamilioni...Tunaomba msiwe wanyonge,wala msioneshe dalili ya kuchoka katika hili ila utayari wa kutupa katiba tunayoitaka aidha mkiwa ndani ya bunge maalumu au nje ya bunge,INAWEZEKANA JAMAA WAKATUMIA RISASI,MABOMU NA MAELFU YA MAASKARI PAMOJA NA NGUVU ZAO ZA KIMAMLAKA KUHAKIKISHA WANAPATA KILE KISICHOKUWEPO KATIKA RASIMU....LAKINI HATUTAFURAHI HISTORIA IKISOMEKA KUWA UKAWA WAMESHINDWA KUTUMIA JUHUDI NA MAARIFA KUHAKIKISHA WANAWAUNGANISHA WATANZANIA KUPATA KATIBA ILIYOTOKANA NA MAONI YAO WENYEWE.....Songa mbele wana Ukawa tupo hatua kwa hatua nanyi.
calvin shemboko