Ujumbe mzito wa Farhan kwa Eng. Hersi Said

kibaigwa finest

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2026
Posts
254
Reaction score
265
Farhan anasema
"Unamuuza Depu na unamruhusu Prince Dube aondoke ndani ya Yanga ambao wote ni Mastreika wazuri, eidha mmoja angebaki na mmoja angeondoka kusikilizia okay unawauza umemleta nani na amefanya nini?

Okay unasajili Allan Okello anakupa performance bora kabisa ndani ya miezi sita unauza Allan kisha unamrudisha out of form Stephen Aziz Ki, yaani timu kutoka kuwa na balance mpaka kupoteza uwiano wa mwendo iliyokuwa nayo ghafla tu. Okay winga mzawa na Mzoefu kama Farid Mussa ameondoka viatu amevaa nani? Anafikia nusu ya Farid?

Ameondoka Mtu mmoja muhimu moja kati ya Madogo waliokuwa Match Analyst hapo Yanga amejiunga na TRA ameenda kuwa Msoma mbinu wao na anafanya kazi kubwa moja kati ya promising talent ameaga na kaenda kuchukua mkataba TRA, hapo bado hujagusa Makocha waliokuwa promising bado wakaondoka Jangwani.

Uje hapo kwenye dimba hapo aliondoka Mhimili wao kwa misimu mitatu tuulizane alipoondoka Mchezaji daraja la Khalid Aucho kuanzia kuusoma mchezo, kuidrive timu una nani mwingine wa daraja lile?. Mudathir is good, Maxi is the best ila itakuwa timu ya kutegemea miujiza yao muda wote? Jibu ni hapana.

Zamani hapo una Fiston ndani nje una Kennedy Musonda, una Feisal ndani nje hapo una Aziz Ki, una Lomalisa ambaye Kibwana anasubiri kwasababu ana uhakika wa rotation, Una Farid anaweza kucheza hapo. Una Aucho, una Watu hapo Mido halafu Sure Boy nae anasubiri dakika, leo hii Sure anatrend kisa kudai? What happened to Young Africans?

Madirisha mawili matatu yaliyopita amekuja Kouma, Assinki, Ecua na wengine wengi tu, nitajieni mara ya mwisho ndani ya misimu mitatu Yanga kaleta Mchezaji hatari kimataifa zaidi ya Allan ni lini? Mara ya mwisho Yanga kaenda usajili kapata Wachezaji hata watatu wameclick ni lini?

Makocha wana shida zao sikatai, lakini kwa timu hii ambayo backbone ni ile ile zaidi ya misimu mitatu tena kwa mpira wa Kiafrika unategemea maajabu? Nimewasifia sana Viongozi wa Yanga wakifanya poa ila katika hili sio mzigo wa Kocha pekee WAO PIA WANA MCHANGO kufikia hapa."
 
Siwezi laumu sana ni Hali ya mchezo tu, ushindani ni mkubwa kulaumu hersinsi busaea mi naona yanga imekamilka Kila idara, shida ushindani alafu siku hizi madaraja yamepungua hata timu za kawaida Zina matunzo mazuri.

Al ahly ya misri mbona haishiriki klabu bingwa, mamelodi katolewa, nasikia hata Orlando kama si kaizer chief nae katolewa hii ni dalili kua wachezaji wanauchovu na kibaya ushindani umeongezeka. Tuwe na subra
 
Farhan Yupo Sahihii, Kocha Alikuwa na Makosa Yake, Na Viongozi Nao Wana Makosa Yao,, Nilishangaa sana Walipomuachia Yule Kocha Miloud Aondoke,, Unamuacha Depu na Okello Waondoke Looh.... !!! Viongozi Wa Yanga Nao Wajitathimini.
 
Farhan Yupo Sahihii, Kocha Alikuwa na Makosa Yake, Na Viongozi Nao Wana Makosa Yao,, Nilishangaa sana Walipomuachia Yule Kocha Miloud Aondoke,, Unamuacha Depu na Okello Waondoke Looh.... !!! Viongozi Wa Yanga Nao Wajitathimini.
Awakuachwa waliuzwa. Ijue tofauti ya kumuacha mtu na kufanya biashara.
 
Huyu mchambuzi ni kolo lia lia, kama kawaida yao makolo hawafichi chuki kwa Hersi😄
 
U
Umemaliza
 
kwa sasa mpira umekuwa wa mitandaoni sana wapo wanaoongea ukweli kwa uhalisia uliokuwepo. Mashabiki wa hizi timu za kariakooo hawataki kuamviwa ukweli wa mapungufu yao kuanzia kwa wachezaji makocha na hata uongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…