Hivi ile mikataba iliyosainiwa baada ya vita ya pili ya dunia haiwezi kuvunjwa?
Nasema hivi kwa sababu japani yupo occupied kijeshi na marekani pia ujerumani yupo occupied na allied (Uingereza, ufaransa, marekani) wakiongozwa na marekani ila wao hawakusaini mkataba.
Sidhani kama Russian wana troops tena ujerumani kwani eastern Germany ilisambaratika 1989 baada ya kufeli kwa siasa za ujamaa zikiongozwa na USSR.
Japan na Germany ni mataifa hatari sana duniani japokua wapo occupied wana maendeleo makubwa sana kiuchumi.
Pia katika Nyanja za michezo ujerumani yupo vizuri sana hasa mpira, kiteknolojia japan na ujerumani wapo njema.
Vita viliwacost sana Germany na japan hasa Hiroshima na Nagasaki baada ya kupigwa na mabomu ya nyuklia.
Napenda kuona hizi nchi zikiwa independent with full sovereignty kwani watakua mbali Zaidi ya hapo walipo.