Hili taifa la Kenya litasambaratishwa na ukabila akitoka Mkalenjin anakuja Mkikuyu,akiondolewa Mkikuyu anaingia Mkalenjin,halafu bila aibu viongozi wa kitaifa (wabunge,magavana,maseneta )bila aibu wanasimama na kusema watu wetu wamekasirika kwa kuondolewa mmoja wetu katika nafasi ya juu,utafikiri hayo ndio yaliyowafanya wapigiwe kura,kwani akiteuliwa huyo mtu kutoka kabila lako ndio wengine watafaidi hiyo keki?sana sana watakaofaidi huo uteuzi ni familia yake na jamii yake,akiwa kwa madaraka anakula peke yake akitolewa mnataka kabila lote liandamane,hebu jifunzeni na mubadirike UKABILA unaangamiza taifa lenu.