Patrick Elias
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 332
- 108
Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu mapenzi ya jinsia moja.
Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Isaac Mumena anasema kuwa Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua.
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Vikwazo vyenyewe ni pamoja na kufutilia mbali msaada wa kijeshi, kuwapiga mrufuu baadhi ya maafisa wa serikali kusafiri nje na kupiga tanji mali zao.
Maandamano kupinga mapenzi ya jinsia mopja na kumpongeza Rais Museveni kuwa kupitisha sheria hiyo
Kadhalika msemaji wa serikali Ofwono Opondo amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa wananchi wa Uganda wanafahamu kuwa hawatategemea tena msaada wa nchi za Magharibi
Sheria hiyo iliyotiwa saini na Rais Yoweri Museveni mwezi Februari inasema kuwa wanaopatikana na hatia mara mbili ya kuhusika na mapenzi ya jinsia moja watafungwa maisha jela.
Sheria hiyo pia inaharamisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja pamoja na kuwataka wananchi kuwashitaki watu wanaohusika na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa maafisa wakuu.
Ikulu ya White house imelaani sheria hiyo ikisema kuwa inakwenda kinyume na uhusiano kati ya nchi hizo ikitoa wito wa sheria hiyo kufutuliwa mbali.
Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amefananisha sheria hiyo na sheria za utawala wa zamani wa kinazzi nchini Ujerumani.
Unajua mie nashindwa kuzielewa hizi nchi za Afrika kwa jinsi zinavyoshupalia sana suala la ushoga, hadi kukosana na haya mataifa na kusema hata misaada wanayoitaka sana basi. Binafsi ushoga naupinga kwa msimamo thabiti wa kidini, lakini sintakuwa wa kwanza wala wa mwisho kumtupia jiwe mtu aliye shoga.
Sasa ninachojiuliza, kwani hawa mawaziri wanaopigia kelele ushoga kwa nguvu zote, wasipoweka sheria ya ushoga nchini wataombwa au kuliwa wao na hao mashoga? Hawa mawaziri wanawaogopa mashoga? Kwa nini kwa mfano, hatushupalii uchangu doa kama vile tu ushoga, ina maana uchangu doa ni halali?
Kuna mambo mengi ya faida kubwa yanayotaka tuyashupalie kwa sheria kali kama kunajisi watoto wadogo, kuuwawa kwa albino, rushwa, ujangili, madereva walevi, wizi wa hela za umma, ukosefu haki katika ajira nk, lakini sie tumeshupalia ushoga utafikiri tumeambiwa wazungu wanataka kuja kutufanya kitu mbaya nyuma. Kisa ni nini hasa? Waache mashoga wajiue kwa raha na mashoga wenzao, kwani sisi tusio mashoga inatuhusu nini?