ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 951
UFISADI BODI YA KAHAWA MOSHI
Wana JF, hii ni taarifa iliyotumwa na Mwanajamii mwenzetu kupitia mtandao binafsi, kama kuna mmoja wetu anawea kufuatilia na kutupa ukweli wa habari hii, tafadhali ashughulikie na kuyaweka hewani yatakayojitokeza kwa manufaa ya nchi yetu, Naileta kwenu taarifa hii kama ilivyopokelewa:
Wana JF, hii ni taarifa iliyotumwa na Mwanajamii mwenzetu kupitia mtandao binafsi, kama kuna mmoja wetu anawea kufuatilia na kutupa ukweli wa habari hii, tafadhali ashughulikie na kuyaweka hewani yatakayojitokeza kwa manufaa ya nchi yetu, Naileta kwenu taarifa hii kama ilivyopokelewa:
Kwenye gazeti la Mwanachi la tarehe 16 Apili 2008 iliandika habari ya kusikitisha kuhusu kupigwa mnada kwa jengo la kahawa lillopo Moshi linalomilikiwa na Bodi ya Kahawa (TCB) kutokana na deni la Tshs. 700 milioni inayodaiwa na Benki ya Exim.
Tafadhali tunaomba vyombo vya habari vifuatilie suala hili kwa kina ili kujua:- (i) ni kampuni gani iliyodhaminiwa huo mkopo na Bodi ya Kahawa ambayo ni chombo cha umma kinachotegemea bajeti ya seriklai kwa asilimia mia moja na hakiruhusiwi kufanya biashara (i) wamiliki wa kampuni iliyochukua mkopo ni akina nani, na wana mahusinano gani na Bodi mpaka iwadhamini mkpo mkubwa kiasi hiki (iii) nani aliidhinisha Bodi itoe jengo la wakulima la thamani ya mamilioni kudhamini mkopo ambao maslahi yake kwa wakulima hayajulikani (iv) Bodi/wakulima wa kahawa wamenufaikaje na mkopo uliotolewa na Benki ya Exim kwa kampuni iliyodhaminiwa (v) Mkataba unasemaje na nani aliyesaini mkataba huo na kwa idhini ya nani
..????, Je serikali ilikuwa inajua haya mapema??/
Inasikitisha sana kuona viongozi wa nchi hii hasivyokuwa makini na umaskini wa watu wao, inaumiza sana, mtu anapewa dhamana na anaitumia kwa maslahi yake binafsi na familia yake!!!!. Tafadhali tunaomba suala hili lichunguzwa kwa makini. Kuna taarifa za kuthibitika kuwa jengo hilo liliwekwa dhamana na iliyokuwa menejimenti ya Bodi ya kahawa kinyemela na hakuna faidia yeyote kwa Bodi hiyo kutokana na Mkopo uliochukuliwa toka Exim Benki. Taarifa zilizopo ni kuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye sisi tunajua kuwa muda wake wa utumishi ulikwisha malizika akaongezewa tena pasipo ufanisi, aliliweka rehani jengo hilo kwa manufaa binafsi ili ajipatie kiasi cha Tshs. 300 milioni kwa ajili ya Kampuni yake inayoitwa African Consulting Group Limited . Hati ya umiliki wa jengo hilo ni No. 4757 LRM lilopo plot Na 52, Manispaa ya Moshi (taarifa zaidi zinajulikana na Mkurugenzi Mkuu huyo aliye maliza muda wake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim). Mkurugenzi huyo (jina tunalo) ni mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyoliweka jengo hilo rehani na akiwa mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa alitumia nafasi hiyo na inadaiwa pasipo idhini ya Bodi ya Wakurugenzi wala Serikali (Wizara Kilimo) aliweka rehani jengo ilihali akijua kuwa Bodi ya Kahawa kama chombo cha umma haina maslahi yoyote na mkopo uliochukuliwa toka Benki ya Exim Benki na kampuni yake ambayo taarifa tulizonazo ina milikiwa na watu wanne wengine wawili wanajulikana kwa jina moja tu la Mtani.inasadikika mmoja ni marehemu...
Inasikitisha sana kusema kuwa inawezekana mchezo uliotumika kuliweka jengo hilo rehani hautofautiani na ufisadi, kwani japo kuwa jengo hili linamilikiwa na Bodi ya Kahawa na lilijengwa kwa michango ya wadau wa kahawa kiiwemo chama kikuu cha wakulima wa kahawa Mkoani Kilimanjaro, (KNCU), wahusika hawakufahamishwa na pia hata Benki ya Exim ilikubali kuingia kwenye ufisadi huu pasipo kuwepo kwa ridhaa ya Bodi ya wakurugenzi wala Serikali. Ikumbukwe kuwa Exim Benki iliwahi kuhusika siku za nyuma na kushindwa kulipa deni la Mfuko wa Pembejeo wa Taifa na sijui mpaka sasa kama wameshalipa!.
Tunazo taarifa kuwa usajili wa rehani ilifanyika kwa msajili wa ardhi kwa jina la mkopo uliochukuliwa na kampuni ya African Consulting Group Limited . inayomilikiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi na yeye ndie aliyewasilisha maombi ya Mkopo Benki, alisaini Mkataba wa Mkopo na wakati huo huo kusaini Hati ya Rehani kwa nafasi ya Mkurugenzi wa Bodi ya Kahaw, kudhamini mkopo uliochukuliwa na kampuni yake binafsi!!!!. Ni wazi kuwa Benki ya Exim(T)Limited ilikuwa inafahamu mchezo uliokuwa ukiendelea kwenye suala hili na kwa nia ya kujinufaisha kwa jasho letu wanyonge ikafumba macho. Hii Benki ya Exim inauzalendo kweli japo kuwa inajifanya kuwasaidia wakulima???????...
Ili kunusulu jengo letu sisi maskini, tunaomba sana suala hili lichunguzwe kwa kina kujua ukweli kuhusu ufisadi uliofanyika na ikiwezekana kuwachukulia hatua wahusika. tunatumaini ukweli utajulikana haraka toka ndani ya Bodi ya Kahawa hususan Mwenyekiti wa Bodi, Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo, na aliyekuwa Mkuruhgenzi Mkuu wa Bodi, Wizara ya Ardhi, ofsi za Moshi ambapo Mkataba wa Rehani (Mortgage) ulisajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi, Menejimenti ya Exim Bank pamoja na Chama cha Ushirika cha wakulima wa Kahawa Mkoani Kilimanjaro, (KNCU). Kwa ufisadi huu Tanzania tunakwenda wapi!