UDOM kwanini mnatoa transcript feki?

kigumbe

Senior Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
168
Reaction score
63
Kwa muda mrefu wahitimu wa chuo kikuu cha Dodoma wamekuwa wakilalamikia uongozi wa kitivo cha Elimu kutoa matokeo ya wanafunzi yaani mwaka wa tatu kwenye karatasi za kawaida A4 na printing ya black and white.

Ni aibu kubwa sana kwa mambo haya ya ajabu ukizingatia chuo hiki ni kikubwa kwa majengo Afrika mashariki na Kati Ila kwa mambo haya yanazalilisha ubora wa chuo hiki cha Elimu.

Wadau wa Elimu mkiona transcript za graduants wa Dodoma UDOM ni aibu maana hata picha ya mtu husika kwenye cheti haonekani vizuri hii tu ni ufisadi wa chuo hiki amabacho siasa ndo msingi wa uongozi na utendaji wake.
 
Sio kitivo cha elimu pekee, ni vitivo vyote wanatoa transcripts za namna hiyo. Sema tu wengine huwa wanaprint coloured. Lakini wengi huprint black and white.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…