Tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani na sera ya uchumi wa viwanda, upande wa upinzani umekuwa ukibeza.
Mbaya zaidi ni maneno na lugha inayotumiwa humu na wafuasi wa kauli hizo za kubeza za viongozi wao, kiasi cha kuita viwonder.
Narejea baadhi ya Sera ya viwanda na biashara iloyomo kwenye Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, ili kukumbushana kinachoendelea kutekelezwa.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015–2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuweka nguvu kubwa katika kukamilisha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu (2010–2020) ambayo malengo yake ni kuiwezesha Sekta ya Viwanda kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu kama ilivyoanishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Aidha, Utekelezaji wa Ilani hii utakuwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16-
2020/21) ambao lengo lake ni kuendeleza uchumi viwanda. Katika kipindi hicho, utaanza ujenzi wa viwanda mama (basic industries) na kuimarisha viwanda vilivyopo.
Ili kufikia lengo hilo, mipango na mikakati ni kama ifuatavyo:
1) Maeneo Maalumu ya Uwekezaji:
(i) Mikoa 20 imetenga Maeneo Maalumu ya Uwekezaji ili yawekewe miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga viwanda na kufanya biashara katika maeneo hayo.
(ii) Sheria za Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ) na Maeneo Maalumu ya Uchumi (SEZ) zimepitiwa ambapo vivutio mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafuu ya kodi vimebainishwa ili kuhamasisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika uwekezaji.
2) Benki ya Rasilimali imeanzisha Dirisha Maalumu kwa ajili ya kuwezesha wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kupata mikopo
kwa riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda:
3) Jumla ya makampuni 130 yamewekeza mitaji yenye thamani ya Shilingi bilioni 2,041.6 mwaka 2014 ukilinganisha na Shilingi
bilioni 126.6 mwaka 2010 na kutengeneza ajira za moja kwa moja zilizotokana na uwekezaji huo kufikia 31,923; na
3) Ekari 107 zimepimwa katika Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuanzisha Vijiji vya Viwanda (Industrial Villages) na kupata hati miliki (Title Deeds) ili kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengeneza
bidhaa za ngozi.
Kila mmoja wetu amejipangaje kufikia lengo la uchumi viwanda au ndiyo tunaishi katika msemo wetu wa kizembe kwamba ngoja tuone! Ngoja ngoja huumiza matumbo au Chelewa chelewa utakuta mtoto si wako.
Naamini msingi wa kejeli za viongozi wa upinzani ni wao kutokuwa na sera mbadala kuhusu uchumi kwa sababu hawajui vichecheo vya kukua kwa uchumi.
cc:
Makene
Mwanahabari Huru
Daudi Mchambuzi
Salary slip
Francis12
BAK, nk