Uchumi wa viwanda

EL Team 2015

Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
61
Reaction score
51
Ndugu ,Watanzania baada ya shughuli nyingi za kisiasa ni muda muafaka sasa kwa sisi kwa umoja wetu kurudi na kuendelea kufanya kazi ili kuimarisha uchumi wetu.

Uchumi wetu kwa maana ya MTU mmoja mmoja na kaya kwa ujula wake . Uchumi imara utatupa nguvu ya kimaamuzi na maendeleo ya kisiasa na kisera .

Tumezungunzia Suala la Elimu ,Elimu ,Elimu wakati tukiomba kura hiki ni kipindi kingine ambacho tunapaswa kuangalia mustakabali wetu na taifa letu kiuchumi.

Nimeona kwamba kwa sasa kuna vijana wengi wasomi na ambao kweli hawakua na fursa ya Elimu itakaowawezesha kuajiriwa kwenye white color jobs. Ila ni jukumu letu kwa pamoja kuangalia fursa zilizopo na kuanza kuzifanyia kazi kwa kuleta maendeleo ya pamoja .

Katika hili nimeonelea kuleta wazo tofauti kidogo baada ya Shule za kata ninafikiri ni muda sasa Wa kuangalia jinsi kila kata itakavyoweza kuwa na kiwanda na jinsi ya kukiendeleza .

Hili litaangaliwa kwa kuandaa michanganua ya maligafi zinazopatikana sehemu husika na kwa Tanzania yetu kila sehemu kuna maligafi inayopatikana kwa mfano sehemu zinazolimwa miwa kwa wingi kama sio kiwanda cha sukari basi watu wanaweza kujiunga na kuwa na viwanda vidogovidogo vya kukamua juice ya miwa na kuipaki vizuri kibiashara na itakua na tija kwenye kuzalisha ajira na kukuza uchumi Wa taifa letu.
 
Nna hamu sana kuzungumzia swala la uchumi wa viwanda. Ila itabidi niandae maelezo marefu sana so ntajibu kwa kifupi hapa ku mention strategies za industrialization na labda nikishaandaa maelezo marefu ntayaweka hapa pia.

Huwa wanasema hakuwezi kupatikana maendeleo halisi katika nchi yoyote bila kuwa na viwanda. Kwa sababu ni kiwanda ambacho kinaongeza value ya kitu na hivo kimtazamo ni kwamba kiwanda kinafanya multiplication ya output inayozalishwa katika nchi. Mfano ulikuwa unalima ngano lakini ukitengeneza kiwanda cha kusaga ngano na kuoka mikate utakuwa umeongeza thamani maradufu, na hiyo ndio haswa faida ya viwanda.

Katika nchi zetu za kiafrica baada ya ukoloni serikali nyingi ziliweka strategies mbali mbali za kuindustrialize. Na ni kupitia strategies hizi hizi ndipo haswa hata kwa sasa tutaweza tena revise sera ya viwanda maana kuna somo kubwa ni kwa nini strategies hizo zilifeli.

Kwa sasa ntaorodhesha tu hizo strategies za industrialization ambazo kwa upande wangu mimi naona bado zina apply mpaka sasa kama serikali kweli imejizatiti kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.

1) Import-substitution industrialization
2) Integrated rural development -- hii ni strategy ambayo inalenga zaidi kuimarisha kilimo vijijini na ku encourage watu wa vijijini wajihusishe na shughuli ndogo ndogo za kuzalisha vitu nje ya kilimo mfano viwanda vidogo vidogo vya ususi, uchongaji, ukamuaji mafuta ambazo pia ni msingi mzuri wa kuinua shughuli za viwanda. Kama ukifatilia industrialization ya western countries utaona ni jinsi gani wali move from Feudalism to Capitalism.
3) Structural adjustment programs (Privatization)
4) Export oriented industrialization mfano kitu kama EPZA
5) Industries industrialization- hapa ni kuwa na viwanda vya kutengeneza malighafi kwa ajili ya viwanda vingine. Mfano kama SIDO wanavotengeneza mashine kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo.

I wish ningedadafua zaidi ila sina energy ya kutosha but ntazidi kufanya editing nielezee kila strategy hapo juu na namna gani inaweza kufanya Tanzania iwe ya viwanda kwa miaka 15 ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…