Ule muda tuliokuwa tunaungoja sasa umewadia. Ni haki yetu ya kikatiba kutimiza wajibu wa kuchagua kiongozi bora ambaye ataweza kutuvusha hapa tulipo.
Ni vyema tukikumbushana kwamba yapo maisha baada ya uchaguzi... Kwani sote tu Watanzania, lengo ni kujenga TANZANIA yetu sote. Tusibaguane kiitaikadi wala kwa vyama, tudumishe umoja wetu na mshikamano wetu.
Mungu ibariki TANZANIA...