Ubaguzi waendelea Marekani

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Ubaguzi waendelea Marekani, mwanahabari wa CNN akamatwa akiripoti mubashara

May 30, 2020 03:46 UTC

[https://media]

Polisi nchini Marekani wameendeleza vitendo vya kuwabagua Wamarekani wenye asilia ya Afrika na mara hii mwanahabari wa Televisheni ya CNN amekamatwa akiwa anarusha ripoti hewani mubashara kuhusu ghasia za kupinga ubaguzi wa rangi huko Minneapolis.

Kwa mujibu wa taarifa Omar Jimenez, mwanahabari wa CNN alikuwa anarusha hewani ripoti mubashara kuhusu ukatili wa Polisi ya Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wakati alipotiwa mbaroni na polisi.

Katika tukio hilo la Ijumaa Omar Jimenez, ripoti Mmarekani Mwenye Asili ya Afrika akiwa na timu yake walikamatwa na kuzuiwa kurusha hewani ripoti kuhusu ukatili wa polisi ambao umeibua ghasia na machafuko mjini Minneapolis.

Watu wa Minneapolis wanaandamana kupinga ukatili wa polisi wazungu wambao walimuua kinyama Mmarekani mweusi au mwenye asili ya Afrika.

[https://media]Polisi wa Marekani akiwa amemkanyaga Floyd na kumuua

Katika mauaji mapya ya kibaguzi ya polisi wa Marekani Jumatatu iliyopita afisa mmoja wa polisi mzungu alimuua kwa namna ya kikatili George Floyd (46) Mmarekani mwenye asili ya Afrika kwa kumbana shingo kwa goti la mguu wake wa kushoto. Floyd alikuwa akipiga kelele kwa kusema: "Umenibana shingo siwezi kupumua," "naomba maji" na "usiniue" hadi alipofariki dunia. Kufuatia ukatili huo wa kutisha, meya wa mji wa Minneapolis, Jacob Frey amewafuta kazi maafisa wanne wa polisi kwa kusababisha kifo cha Floyd. Kufuatia jinai hiyo, wakazi wa mji wa Minneapolis, jimbo la Minnesota wamefanya maandamano makubwa ya kulaani jinai hiyo huku wakitaka wahusika wachukuliwe hatua kali. Katika maandamano hayo Mmarekani mwingine mweusi ameuawa kwa kupigwa risasi mjini hapo.





Sent from my JSN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Taarifa yako ya kishamba ina maneno mengi yanayojirudia rudia.
Rudi elementary school
 
Naombeni connection ya ndugu zake wanapoishi nataka nikalipize kisasi
 
US taifa lakibaguzi sana linalojificha katika kigenge chakujifanya mtetezi wahaki zabina adamu wakati yeye ndie anaeongoza kwakuzikiuka

:-US labda anaongoza katika utetezi wahaki zamashoga nawasagaji
 
we jamaa bana umeshindwa kutumia akili kung'amua hiyo kofia ya make whites great again imefanywa makusudi kupaka matope ile ya Make America Great Again ya Trump ili ionekane ya kibaguzi

Halafu mbona unaonekana una agenda, hayo mapicha sijui ya Waafrika wanateswa hayo mbona yanafahamika, na Waafrika wameteswa na kufanywa watumwa hata na Waarabu kiasi c ha kupelekea kule Zanzibar kuchinja Waarabu karibia wote kama kuku kutokana na hasira za kuteswa na kubaguliwa?
 
US taifa lakibaguzi sana linalojificha katika kigenge chakujifanya mtetezi wahaki zabina adamu wakati yeye ndie anaeongoza kwakuzikiuka

:-US labda anaongoza katika utetezi wahaki zamashoga nawasagaji
arafu viongozi wetu wanawaona ndio kama miungu
 
jidanganye hivyo hivy
 
Muafrika hata asipobaguliwa atajibagua mwenyewe,waafrika tumekua na tabia ya kubaguana kidini,kikabila,kisiasa,kiitikadi,kitaifa,kiajira.
Leo kwanini muafrika asibaguliwe,kwanini muafrika asiteswe katika mataifa mengine,kuwa muafrika nje ya Afrika si kosa,kosa ni kuwa muafrika ndani ya Afrika na kushindwa kuitunza thamani ya muafrika mwenzake.
Tutabaguliwa sana hadi akili zikae sawa.
 
aseee acha tu MKUU waafrika lazma tubadilike.....

Sent using My COVID-19
kubadirika haiwezekan kwasababu ushakuwa ulemavu wetu. mfano mh magufuri alivyi pishana nao katika maamuzi si unaona viongozi wengine walivyomkosoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…